Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)

Hizi hapa sifa na bei ya Apple iPhone SE (2020)
Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020) Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye kampuni ya Apple hapo jana imezindua simu mpya ya iPhone SE (2020). Simu hii inakuja kama toleo la bei nafuu la simu za iPhone ambazo zilitoka hapo mwaka jana (2019) na kwa upande mwingine unaweza kusema simu hii inakuja na muonekano na sifa kama za iPhone 8.

Advertisement

iPhone SE (2020) inakuja na kioo cha inch 4.7, kioo ambacho kinakuja na teknolojia za Retina HD, True Tone pamoja na uwezo wa Dolby Vision na HDR10. Kwa mbele simu hii inakuja na sehemu ya fingerprint ambayo inapatikana kwa chini ya simu hiyo.

Kwa upande wa juu iPhone SE (2020) inakuja na kamera moja ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 7 huku ikiwa na teknolojia za Face detection, HDR, na panorama. Kamera hiyo ya mbele pia inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080 @30fps; gyro-EIS.

Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)

Kwa upande wa nyuma, iPhone SE (2020) inakuja na kamera mmoja ya Megapixel 12 ambayo hii ni wide lensi, kamera ambayo inakuja na teknolojia ya HDR pamoja na uwezo wa kurekodi video hadi za 4K. Hii ni sawa na kusema iPhone SE (2020) ina uwezo wa kurekodi video za hadi pixel 2160@ 24/30/60fps (frame per second).

Kwa upande wa sifa za ndani, simu hii mpya ya iPhone inakuja ikiwa inaendeshwa na processor mpya ya Apple A13 Bionic processor ambayo inakuja na idadi ya cores sita (Hexa-core) zenye jumla ya speed ya hadi 2×2.65 GHz Lightning + 4×1.8 GHz Thunder. Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 64, GB 128 na GB 256. Simu hii haina sehemu ya kuongeza uhifadhi kwa kutumia memory card.

Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)
Kwa upande wa battery iPhone SE (2020) inakuja na teknolojia ya fast charging yenye uwezo wa hadi walt 18, ambayo inadaiwa kuchaji simu hii hadi asilimia 50 ndani ya dakika 30. Battery ya simu hii inakuja na uwezo wa 1821 mAh battery (6.96 Wh), battery ambayo inafanana na ile ya iPhone 8.

Kwa upande wa bei, iPhone SE (2020) inakuja ikiwa inauzwa dollar za marekani $399 ambayo ni sawa na Tsh 929,000 bila kodi kwa toleo la GB 64. Huku toleo lenye GB 128 likiwa lina patikana kwa dollar za marekani $449 ambayo ni sawa na Tsh 1,042,000 bila kodi, huku toleo la mwisho la GB 256 likiwa lina patikana kwa dollar $549 ambayo ni sawa na Tsh 1,274,000 bila kodi. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.

Makala hii imeongezwa tarehe 17-April kuonyesha uwezo wa battery ya iPhone SE (2020), pamoja na uwezo wa RAM ya simu hii.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use