Hivi karibuni instagram inategemea kuleta mabadiliko mapya, mabadiliko ambayo yanaweza kuwa mabadiloko mazuri sana kwa watumiaji wa sehemu ya Insta Live.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, Instagram kwa sasa inafanya majaribio ya kuja na sehemu mpya ambayo itaruhusu watumiaji wa Insta Live, kuweza kuhifadhi video zao za live kwenye IGTV mara baada ya kumaliza kuchukua video.
Kipindi cha nyuma kulikuwa hakuna njia ya moja kwa moja ya kushare video za live, ijapokuwa kuna mbinu mbalimbali ambazo unaweza kutumia kuhifadhi video hizo. Sehemu hiyo mpya ya kuhifadhi video hizo za live, itakuwa ipo kwenye mfumo wa “kitufe maalum” ambacho utakuwa ukikitumia mara baada ya kumaliza kurekodi video hizo za Insta Live.
Kama unavyoweza kuna hapo juu, utaweza kuona sehemu mpya ya Share to IGTV, sehemu ambayo itakuwa ikitokea mara baada ya kumaliza kuchukua video za insta Live. Pia vilevile mbali ya uwezo wa kushare video hizo, pia utapata uwezo wa kushare video fupi “Preview” kwenye ukurasa wako wa instagram wa kawaida ili kuruhusu watu kugundua video ya kwa urahisi.
Hata hivyo, sehemu za maswali ambazo zitakuwa zinatumiwa pamoja na comment zote hazito kuwepo kwenye video hizo mara baada ya kuwekwa kwenye sehemu ya IGTV.
Instagram kwa sasa inaonekana kutumia muda huu kukuza sehemu ya IGTV na mtandao wa instagram kwa ujumla, muda ambao watu wengi kwenye nchi mbalimbali wako nyumbani na wanatumia mtandao huo kuchukua video za live kwenda kwa watu mbalimbali.
Hivi karibuni instagram iliwezesha uwezo wa kusoma meseji za DM kupitia kompyuta, sehemu ambayo hadi sasa tayari inapatikana kwa watumiaji wote wa Instagram dunia nzima. Kama wewe unatumia kompyuta basi jaribu kuingia kwenye tovuti ya instagram.com kwa kutumia kompyuta yako na utaweza kutumia mtandao huo kama unatumia application.