in

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)

Hizi hapa biashara ngumu kufanya mtandaoni kwa sasa hapa Tanzania

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)

Katika hali ya kawaida ni muhimu kujua pande mbili za kila kitu, iwe ni pande nzuri na hata pende mbaya, kwa kuwa hapa Tanzania tech tumekuwa tukiongelea zaidi pande nzuri hebu leo tuchukue muda kidogo na kuangalia pande ambayo sio nzuri sana kibiashara.

Kupitia makala ya leo nitaenda kuongelea aina za biashara ambazo kwa mtazamo wangu naona sio nzuri sana kufanya mtandaoni kwa mwaka huu 2020. Kupitia hapa nitajitahidi kuwa na maneno machache lakini nikufikishe pale ambapo ninataka ufukie. Makala hii ina lengo la kuonyesha changamoto za aina fulani za biashara ili kusaidia mtu anaetaka kuanza aweze kujipanga.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa kusema hayo basi moja kwa moja twende kwenye makala yetu hii na ninatumaini wote tutaenda kujifunza kwa pamoja.

Biashara ya Tovuti ya Kuuza na Kununua

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)

Moja kati ya biashara ambayo imekuwa ikitamaniwa na wengi ni biashara ya kuuza na kununua, hii ni kwa sababu watu wengi waliona mafanikio ya biashara fulani hivyo kuamua kuanzisha biashara kama hii ili kufanikiwa kama hizo biashara au pengine hata zaidi. Lakini pamoja na hayo ni wazi kuwa biashara hii sio nzuri kufanya mtandaoni kwa mwaka 2020 na zifuatazo ni sababu za msingi.

  • Uwezo wa Mitandao ya Kijamii na Ads

Kadri muda unavyo kwenda unakubaliana na mimi kuwa watu huamua kuuza zaidi vitu kupitia mitandao yako ya kijamii kuliko hata kupitia kwenye mitandao ya kuuza na kununua. Hii inatokana na urahisi wa kufikia watu wengi zaidi hasa pale mtu anapokuwa na wafuasi wengi zaidi. Pia siku hizi zimekuja kurasa ambazo unaweza kutuma picha na mtu akaweka tangazo lako na kuandika bei yake na bidhaa inapo uzika basi ukupa pesa yako na yeye kuchukua pesa yake.

Mbali na hayo pia matangazo au Ads kwenye mitandao ya kijamii yamekuwa na uwezo wa kufanya bidhaa yako kuwafikia watu wengi zaidi, hii inatokana na urahisi wa kulipia kupitia Mastercard mbalimbali pamoja na wingi wa watu kwenye mitandao ya kijamii tofauti na kwenye tovuti nyingine.

  • Ngumu Kutengeneza Kipato

Lakini hiyo sio sababu pekee, sababu nyingine ni kuwa ni ngumu sana kutengeneza kipato kupitia biashara ya tovuti ya kuuza na kununua. Hii ni kwa sababu watu wengi hutegemea kuuza vifurushi ambavyo huwapa wateja nafasi za kupost matangazo zaidi au kuruhusu matangazo hayo kukaa juu ya mengine kwa muda fulani na hii pekee haitoshi.

Hiyo ni sababu kuwa njia hizi hazitoshi kumpa mtu sababu ya kuamua kuuza bidhaa yake kwenye mtandao wako tena hasa kama mtumiaji huyu anatafuta njia ya kuuza bidhaa yeke kwa haraka alafu hana pesa ya kulipia.

  • Haitatui Matatizo ya Watumiaji Wote

Hii ni kwa sababu, kwa mfano unayo website yenye watembeleaji 3,000 kwa siku na robo ya hao wakanunua vifurushi vya kufanya matangazo yao yaweze kuonekana juu ya mengine. Hii ni sawa na kusema unao watu 750 ambao matangazo yao yanaonekana juu ya mengine. Hii hufanya wateja ambao hawajalipia matangazo yao yasiweze kuonekana kabisa na hili ni moja kati ya tatizo kubwa sana kwani asilimia kubwa ya watembeleaji wa tovuti hizi ni watembeleaji wa bure na sio wakulipia.

Sababu moja tu, ni wazi kuwa watumiaji wengi wamekuja kwenye tovuti hiyo kwa sababu ya kuuza bidhaa zao ili waweze kujikwamua na matatizo mbalimbali, hivyo ni wazi kuwa asilimia kubwa ya watu hao hawana pesa ya kulipia na hivyo kwa kuweka matangazo juu ya mengine kutafanya wateja hawa kuondoka kwani bidhaa zao hazita weza kuonekana na wateja kwa sababu mteja ataanza kuona matangazo 750 kwanza ndipo aweze kuona yale ya bure.

Mfano mwingine, chukulia ingekuwa unapo ingia kwenye mtandao wa Instagram tu, unaona kwanza matangazo ya post za watu kama post 750 hivi ndipo uweze kuanza kuona post za marafiki zako na watu wengine ulio wafuata (follow).. je unge endelea kutumia mtandao wa instagram.?

  • Wizi Utapeli pamoja na Udanganyifu

Sababu nyingine ni pamoja na kuzuka kwa uwizi, utapeli na udanganyifu kwenye mitandao hii hasa kwa hapa Tanzania. Hii ni kwa sababu mitandao hii imekuwa ikitumiwa na wengi kama sehemu ya kuuza vitu vibovu au vitu ambavyo havifai kwa matumizi ya muda mrefu. Ni wazi kuwa watu wachache sana walio nunua vitu vya kielektroniki vilivyo tumika kupitia mitandao ya kuuza na kununua hupata nafasi ya kudumu na bidhaa hizo kwa muda mrefu sana na hii hutokana na udanganyifu wa wateja wanao uza bidhaa hizo.

  • Kutengeneza Traffic ni Ngumu Sana (Unahitaji kuwa na Pesa)

Mbai na hayo yote hapo juu, kumiliki tovuti ya namna hii kunahitaji uwe na pesa za kufanya matangazo ili kusudi watu waweze kufahamu tovuti yako na kuweza kufanya matangazo. Niwazi kuwa kuwezi kupata traffic kutoka kwenye search engine, hii ni kutokana na ugumu wa post zinazo tengenezwa na watumiaji kuweza kuwa na traffic ya kutosha.

Utakubaliana na mimi kwamba kipindi cha nyuma mtandao wa kupatana ulivuma sana kutokana na kuwepo kwa matangazo mengi sana kwenye TV, Radio na hata kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali. Pia kampuni hiyo ilitumia watu maarufu kutangaza brand yake na hili ni jambo ambalo wote tunakubaliana kuwa lina hitaji pesa tena kwa kiwango kikubwa.

Biashara ya Tovuti ya Habari na Makala Mbalimbali

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)

Aina nyingine ya biashara ambayo ni ngumu kufanya mtandaoni kwa sasa ni biashara ya tovuti ya habari na makala mbalimbali. Sidhani kama kuna mtu hajui ugumu uliopo kwenye kuanzisha biashara ya namna hii, hizi hapa ni baadhi tu ya sababu kwanini biashara hii ni ngumu sana kwa mwaka 2020.

  • Njia za kutengeneza Pesa ni Chache Sana

Moja kati ya sababu kubwa ni kuwa, njia za kutengeneza pesa kupitia tovuti ya habari hasa habari za kiswahili ni ngumu sana. Hii inatokana na kuwepo kwa changamoto ya kampuni kubwa zinazo lipa vizuri zaidi kuwa na sheria ya kutokupokea tovuti za kiswahili.

Hii hufanya tovuti hizi kubakiwa na njia moja tu ya kutengeneza pesa ambayo ni njia ya kuweka matangazo ya ndani ambayo huwekwa na kampuni mbalimbali za ndani ya nchi. Pamoja na kuandika makala ambazo ni sponsored. Na yote haya hayatoshi hasa kwa hapa Tanzania.

  • Gharama Kubwa za Kuendesha Tovuti

Pamoja na kuwepo na uhitaji wa kuwa na watu wa kukusaidia kupost kila siku, pia unahitaji vibali kutoka mamlaka ya mawasiliano vibali ambavyo sio kila mtu ambaye anaweza kupata. Mbali na hayo pia kama una andika habari za ndani ya nchi basi unahitaji timu ambayo itakuwa inatafuta na kuchapisha habari hizo mara kwa mara na hii kufanya gharama za uendeshaji kuwa kubwa zaidi.

  • Unahitaji Kusubiri Muda Mrefu Kufanikiwa

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka biashara ya kufanikiwa haraka sidhani kama biashara hii itakufaa hata kidogo. Kwani biashara hizi zinahitaji uwe mtandaoni kwa muda mrefu na uweze kuaminika kwa watu na mbali ya yote uweze kuwa tegemezi na hayo yote ni mambo yanayo hitaji muda na huwezi kuyapata kama unataka kufanikiwa haraka

Kwa mfano nikisema habari za ndani ya nchi basi moja kwa moja unajua ni tovuti gani ya kutembelea kupata habari hizo na hiyo inakuja baada ya kuona unapata kila habari za ndani nchi kwa urahisi kila siku kupitia tovuti hiyo hiyo.

Hitimisho

Kutokana na urefu wa makala hizi basi naomba ni ishie hapa kwa leo, lakini kama unataka kujua haya zaidi unaweza kutuambia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasisi tutaendelezea makala hii kwa kuongeza biashara nyingine.

Hadi hapo nadhani utakuwa umepata mwanga juu ya vitu ambavyo angalau unahitaji badilisha ii kuwa na biashara bora mtandaoni kama unavyafanya biashara hizo za tovuti ya kuuza na kununua, au kama unataka kuanzisha tovuti ya habari na makala mbalimbali za ndani ya nchi.

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. Nafkiri namimi ni mmoja wapo nnaetaka kuanzisha Tovuta ya nakala mbalimbali sasa nawaza mbinu gani mnisaidie nifanikishe ilo swala ata kama litachukua mda mrefu ,,pia kwa kuongeza biashara ya channel ya Youtube nayo ni ngumu na inahitaji Pesa za kutosha

  2. Hongereni kama timu kwa kujikita kutoa elimu mzuri na ambayo anaye toa anafanikiwa na mlaji atafanikiwa akifuata maelekezo, napenda kutangaza biashara Yangu kwenye fb,watssap pamoja na Instagram nimesoma Maelezo naamini sitaweza kukamilisha bila maelekezo ya vitendo au kufunguliwa