Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Infinix S5 Pro
Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimae hivi leo kampuni ya Infinix imezindua rasmi simu yake mpya ya Infinix S5 Pro. Simu hii ni toleo la maboresho la simu ya Infinix S5 ambayo ilizinduliwa mwaka jana 2019, japokuwa simu hii ni toleo la maboresho lakini muonekano wake haufanani kabisa na toleo la kawaida la Infinix S5 kama ilivyozoeleka.

Infinix S5 Pro inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.53 ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kioo ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 kwa  2220. Kwa mbele simu hii haina kamera ya mbele ambayo ipo juu ya kioo, bali sasa simu hii inakuja na kamera ambayo ipo juu ya simu hiyo na hutoka pale unapotaka kupiga picha au kuchukua video na kurudi pale unapofunga programu ya kamera.

Advertisement

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48 na kamera nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 na nyingine ya mwisho ikiwa ni Low light camera sensor. Kamera zote zina uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps, huku ikisaidiwa na teknolojia za HDR pamoja na panorama. Sifa nyingine za Infinix S5 Pro ni kama zifuatazo.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

 

Sifa za Infinix S5 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.53 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0 yenye mfumo wa OSX
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12nm)
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64
  • Ukubwa wa RAM – GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Pop up kamera Megapixel 16, f/2.0, (wide)
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye nyingine ikiwa na Megapixel 2 na nyingine ikiwa na QVGA. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Violet na Forest Green.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma)

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Bei ya Infinix S5 Pro

Kwa upande wa bei, infinix S5 Pro inategemewa kuanza kupatikana kwanza nchini India na inategemewa kupatikana kuanzia rupee ya India INR9,999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania TZS 313,000 bila kodi.

Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use