Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A11

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy A11
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A11 Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A11

Kampuni ya Samsung imeingiza toleo jipya la simu ya bei rahisi ya Samsung Galaxy A11, simu hii ni toleo kama toleo la muendelezo kwa simu mpya ya Samsung Galaxy A10s ambayo ni ilizinduliwa rasmi mwaka jana 2019.

Galaxy A11 inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya TFT ambacho pia kinakuja na resolution ya pixel 720 x 1560. Kwa mbele juu simu hii inakuja na kamera ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 8 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A11

Advertisement

Kwa nyuma Galaxy A11 inakuja na kamera tatu kwa nyuma, kamera kuu inakuja na Megapixel 13 na kamera nyingine mbili zikiwa na Megapixel 5 na nyingine ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Sifa nyingine za Samsung Galaxy A11 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A11

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya TFT capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset)
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja inakuja na RAM ya GB 2 na nyingine inakuja na RAM ya GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye, f/2.0.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera tatu kwa nyuma, kamera kuu inakuja na Megapixel 13 yenye f/1.8, 28mm (wide), AF. Megapixel 5 yenye, f/2.2 (ultrawide), Megapixel 2 yenye, f/2.4, (depth). Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh, yenye uwezo wa Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, White, Blue, Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa nyuma).

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A11

Bei ya Samsung Galaxy A11

Kwa mujibu wa Samsung, Kwa upande wa bei kama nilivyo kwambia simu hii ni moja kati ya simu ya bei rahisi kutoka Samsung hivyo kwa mujibu wa 91mobile simu hii inategemewa kuuzwa kwa Rupee ya India Rs. 9,990 sawa na takribani Shilingi za Kitanzania TZS 311,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use