Najua kuwa wengi wenu mnatumia simu za Android na kwa sababu hii leo nitaenda kuonyesha njia rahisi sana ambayo itakufanya kuendelea kutumia simu yako Android. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao ulikuwa unatamani kutumia USB Flash kwenye simu yako basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kupitia hapa nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia bila kuhitaji kutu kingine chochote, huna haja ya kununua chochote zaidi ya kuwa na ujuzi mdogo pamoja na baadhi ya vitu ambavyo nitaenda kuonyesha hapo chini. Kumbuka ni muhimu kujua kuwa unaweza kufanya hatua hizi mwenyewe au unaweza ukamuomba mtaalamu yoyote aweze kukusaidia hatua hizi.
Kwa kuanza unahitaji baadhi ya vitu ambayo ni muhimu kuwa navyo, kumbuka vitu vyote vinaweza kupatikana nyumbani kwako au mtaani kwako hivyo usiwe na wasiwasi, pia mahitaji haya yasi kuongopeshe kwani tunachoenda kufanya hapa ni kitu kidogo sana na hakiitaji utaalamu.
- USB cable ya ziada ya smartphone yako, hii unaweza kutumia USB ambayo imeharibika lakini inafanyakazi kwenye kichwa cha kuchomeka kwenye smartphone yako.
- Unahitaji Female USB ambayo hii ni ile ambayo hutumika kuchomeka USB ya kawaida. Unaweza kupata hii kwenye kichwa cha chaji mbovu ya simu ambayo hiafanyi kazi.
- Unahitaji Solder wire, hii inapatikana kwa mafundi wote wa vifaa vya nyumbani pia inauzwa kwenye maduka ya jumla ya vifaa vya kiufundi unaweza kupata popote. Kwenye hatua hizi unahitaji solder wire kidogo sana.
- Pia unahitaji Soldering gun, hii ni ile mashine ndogo ya kuchomelea vifaa vya kielektroniki unaweza kupata kwa mafundi au kwenye maduka ya jumla ya vifaa vya kiufundi au unaweza kupata wauzaji wa vifaa vya kielektroniki.
Sasa baada ya kuhakikisha unavyo vitu vyote hivyo sasa moja kwa moja twende tuka angalie hatua kwa hatua jinsi ya kufanya njia hii rahisi. Kumbuka ni muhimu kufuata hatua zote kama inavyo elekeza kwenye video hapo chini.
Kwa kufuata hatua zote hizo natumaini utakuwa umeweza kutumia USB Flash kwenye smartphone yako, kama unataka njia ya rahisi zaidi unaweza kununua OTG Cable kupitia maduka mbalimbali ya vifaa vya simu yaliyopo karibu na wewe. OTG Cable itakusadia kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako kwa urahisi na haraka.
Kama umependa makala hii kwa namna moja ama nyingine unaweza kupata makala kama hizi kwa kuendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kwa sasa unaweza kusoma hapa jinsi ya kutengeneza kompyuta yako mwenyewe kwa vifaa vya kununua kwa mafundi. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech pia subscribe kupitia channel yetu ya YouTube hapa.
naitaji msaada zaidi kwa sababu na jifunza kompute.
kwani njia hii ni nzuri