Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone

Kwa kutumia njia hii utaweza kutengeneza app ya Android yenye kufanya kazi
Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone

Katika ulimwengu huu ambao simu za mkononi zinatumika kwenye kila kitu ni wazi kuwa, baadhi ya vitu sasa vinawezekana kufanyika bila kutumia kompyuta. Kwa siku ya leo tutaenda kujifunza jinsi ya kutengeneza programu za Android kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Kwa kuanza basi ili kuweza kufanikisha hili unaitaji simu yoyote ya Android pamoja na bando angalau MB 500 au zaidi, hii ni muhimu sababu ni lazima ujaribu kila sehemu ili uweze kupata kile unacho hitaji kwenye app yako hivyo ni muhimu kuwa na bando ya kutosha.

Advertisement

Kama tayari una bando la kutoka basi twende tukaanze somo letu la leo, lakini awali ya hapo labda nikuonyeshe picha za programu ambayo nimetengeneza kwa kutumia simu yangu ya mkononi, unaweza kudownload app hii HAPA ili kujionea mwenyewe.

Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone

Kwa kuanza basi ingia kwenye kisakuzi cha Google chrome kisha ingia kwenye tovuti ya www.andromo.com kishanga utapelekwa kwenye ukurasa maalum, bofya kitufe cha kujisajili au unaweza kutumia mitandao ya kijamii kujisajili.

Baada ya kuhakiki barua pepe yako na kuruhusiwa kuingia kwenye tovuti hiyo, sogea chini kidogo kisha utaona sehemu imeandikwa Create Project, bofya hapo kisha andika jina la App unayotaka kutengeneza kisha bofya Create.

Activities

Baada ya hatua hiyo utaletwa kwenye ukurasa unao anza na Activities, sehemu hii ni muhimu kwani ndio inayokupa nafasi ya kuchagua ni aina gani ya app ambayo unataka kutengeneza. Ni muhimu chagua Activities unayo hitaji kama nilivyo kuonyesha kwenye video hapo juu. Kila activites inayo kazi yake na kazi hizo ni kama zifuatazo.

  • About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
  • Audio Player – Hapa unaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
  • Contact – Hapa unaweza kuweka anwani yako
  • Custom Page – Hapa unaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
  • Email – Hapa unaweza kuweka barua pepe
  • Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
  • Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
  • Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
  • HTML Archive – Hapa unaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
  • Map – Hapa unaweza kuweka ramani
  • PDF – Hapa unaweza kuweka file la PDF
  • Phone – Hapa unaweza kuweka namba ya simu
  • Photo Gallery – Hapa unaweza kuweka picha mbalimbali
  • Podcast – Hapa unaweza kuweka mfumo wa Podcast
  • RSS Feed – Hapa unaweza kuweka RSS fee ya blog yako
  • SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
  • Twitter – Hapa unaweza kuweka ukurasa wao wa Twitter
  • Website – Hapa unaweza kuweka tovuti yako
  • YouTube – Hapa unaweza kuweka ukurasa wako wa Youtube

Muongozo hua hapo juu ndio utakao kusaidia kuweza kutengeneza app yako hivyo weka vitu hivyo kulingana na app yako unavyotaka iwe, kama unataka kutengeneza app ya habari basi unaweza kutumia RSS Feed pia kama unataka kutengeneza app kwaajili ya Youtube Channel yako basi unaweza kutumia sehemu ya Youtube.

Theme

Baada ya kuchagua Activieties sasa endelea kwenye sehemu inayofuata ambayo ni Theme, hapa ni vizuri kuwa makini shuka mpaka sehemu iliyoandikwa Startup Mode kisha chagua Show first activity(no dashboard) kisha bofya Save Changes. Hii itasaidia app yako kuweza kuonyesha kitu ulichoweka kwanza, bila kufanya hivi app yako haitafanya kazi na itakuitaji kuchagua categorie kwanza.

Baada ya hapo upande wa kushoto chagua Navigation, Kwenye sehemu ya Title andika jina la App yako kisha sehemu ya Subtitle andika msemo wa App yako kwa ufupi kwa mfano “pepsi dare for more”, baada ya hapo chini ya Upload a Header Image bofya Choose File na weka picha unayotaka ionekana juu kabisa kwenye app yako, ukimaliza bofya Save Changes.

Global Style

Kupitia hapa utaweza kuchangua rangi ya App yako, changua rangi zote mbili zifanane kati ya Primary Color na Accent Color, baada ya hapo shuka chini kidogo hadi sehemu iliyo andikwa Body Style chagua kati ya Material Light kupata rangi nyeupe kwenye App yako na Material Dark kupata rangi nyeusi kwenye App yako. ukisha maliza bofya Save Changes.

Settings

Kupitia sehemu ya hapa utaweza kufanya mambo ya muhimu sana. Hatua ya kwanza ni kuandika jina la App yako kwenye sehemu ya Name kisha shuka chini kidogo na andika version ya app yako, alafu shuka tena chini kidogo mpaka mahali palipo andikwa Target Market, hapa ni vyema kuwa makini na kuchagua Play Store kama unataka kuweka app yako Play Store na pia unaweza kuchagua Samsung Apps au Amazon Appstore kama unataka kuweka app yako kwenye masoko hayo.

Baada ya kuchagua Target Market shuka chini kidogo kwenye Category kisha chagua aina ya App ambayo unataka kutengeneza, chini yake kwenye sehemu ya Description hapa utajaza maelezo yoyote kuhusu App yako na kama huna malezo yoyote basi unaweza kuacha wazi. Baada ya kumaliza kuweka maelezo ya App yako kwa pembeni chagua sehemu iliyoandikwa App Icon.

Sehemu hii ni muhimu kwani hii ndio picha ya App yako hivyo kama tayari unayo picha ya App yako sasa ndio wakati wa kuiweka na uta bofya sehemu iliyo andikwa Choose File kisha chagua picha unayotaka ndani ya simu yako, hakikisha picha yako ina ukubwa wa 512 x 512 na iwe na format ya PNG. Baada ya kumaliza hatua hiyo shuka mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huo kisha bofya kitufe cha Save Changes.

Services

Kama nilivyo kwambia kwenye video hapo juu, sehemu ya Monetization, hii inafanya kazi kwa watu wenye akaunti za kulipia. Kama unatumia akaunti ya bure sehemu hii haiwezi kufanya kazi kwenye app yako. Ndio maana tume endelea kwenye sehemu ya Services. Sasa ili kuweka Notification kwenye app yako unaweza kufuata maelezo kwenye tovuti ya Andromo Hapa.

Baada ya hapo malizia kwa kurudi juu kisha bofya sehemu ya Build kisha kisha chagua sehemu iliyoandikwa Build My App.

Subiri mpaka programu yako ikamilike kisha utaona sehemu ya kudownload chini yake au barua pepe ambayo itakuwa na programu yako ya Android, download app yako na ijaribu ili kuona kama inafanya kazi inavyotakiwa. Somo linalofuata nitakuelekeza jinsi ya kuweka App hi kwenye soko la Play Store ikifuatiwa na jinsi ya kuweka App hiyo kwenye soko la Amazon Store.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

46 comments
  1. aise pindi nimelielewa lakini ujaelezea kitu kimoja kuusu kupost kitu kwenye app ulio tengeneza naomba tuwasiliabe 0755471946

  2. Nilikua nauliza kuhusu kuandika username katika kujisajiri nimejaribu ila inakataa..
    Je unaeza npa mfano wa jina ambalo wao wanalihitaji

  3. jee naweza nikaiunganisha hiy app niliyoitengeneza kwenye blog ili posti za kutoka kwnye blog yangu ziwe zinaingia kwenye app automatically

  4. app nmetengeneza lakn ina sehemu ya about tu hamna kitu kngne sasa na kupost itakua pale kwenye activity nmekosea kuhusu kujaza maana hata sielew najaza nn

  5. Kwanza niwape pongezi kwa maelezo yeah mazuri, sema ninachotaka kujua ni kwamba!!, nitawekaje ama nitapostije mambo yang kwenye hiyo app ili mtu akiidownload aweze kuona na Haina gharama kwa upande Wa Jodi-TCRA!??

  6. broh,,, nmetengeneza app keaajiliya site ya music,,

    shida niipatayo ni wakati wa kudownload nyimbo inakubali lakin ikishadownload.. kinachotokea sio wimbo tena ni attachment/document (mfumo wa maandish )naomba kujua ni nin sababu na naisolve vp

  7. Hongereni kwa kazi nzuri,
    naomba kujua, kama inawezekana kutengeneza app ya biashara yaani na sehemu ya malipo iwepo, je ni salama kwa kutumia njia hii ama mpaka kutengeneza kwakutumia coding? pia kuendesha app ya namna hiyo inahitaji vibali malipo ya kodi?
    Nashukuru kwa atakaye nisahidia kunijulisha

  8. apps imeshajitengeneza but nahis sjaelewa nikitaka kutuma kitu kwenye io app ndio sielew…unawezà kunielewesha

  9. Ukwer nimeioenda kazi yako lakin mm kilicho ni shinda no kwenye kulipia il nifungue app MSAADA wako kunielekeza jins ya kufanya

  10. Labda naomba nijue umetengeneza app imefanikiwa je faida niipi?nakama Ina faida unaweza kutuelezea

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use