Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9

Simu ya bei nafuu yeye uwezo mkubwa wa kudumu na chaji
Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9 Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9

Baada ya tetesi za ujio wake siku za karibuni, hatimaye hivi leo kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix Hot 9. Simu hii ni toleo la maboresho la simu ya Infinix Hot 8 ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka jana 2019.

Tukianza kwa mbele, Infinix Hot 9 inakuja na kioo cha inch 6.6 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kioo hicho kina kuja na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution hadi pixel 720 kwa 1600. Kwa juu ya kioo hicho kuna kamera moja ya Selfie yenye Megapixel 8 ambayo pia inauwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9

Advertisement

Kwa nyuma Infinix Hot 9 inakuja na kamera nne, kamera kuu ya simu hii ikiwa na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na uwezo wa Megapixel 2, na moja ya mwisho ikiwa na Megapixel 0.3 (VGA kamera). Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Ili kupiga picha vizuri hasa wakati wa usiku Infinix Hot 9 inakuja na Flash nne za LED ikiwa pamoja na teknolojia ya AI inayofanya picha kuonekana vizuri zaidi.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9

Kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Hot 9 inakuja na processor ya Mediatek MT6762D Helio A25, processor inayosaidiwa na CPU yenye speed hadi Octa-core (4×1.8 GHz Cortex-A53 & 4×1.4 GHz Cortex-A53). Kwa pamoja simu hii inasaidiwa na RAM ya GB 3 au GB 4 kulingana na chaguo lako.

Infinix Hot 9 inakuja kwa matoleo mawili tofauti toleo la kwanza likiwa na uhifadhi wa ndani wa GB 128 na toleo la pili likiwa linakuja na uhifadhi wa ndani wa GB 64. Kama hiyo haitoshi unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card ya MicroSD Card ya hadi GB 256.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 9

Kwa upande wa battery, Infinix Hot 9 inakuja na battery kubwa ya mAh 5,000, battery ambayo ina uwezekano mkubwa wa kufikisha siku nzima bila kuchaji simu yako. Mbali na hayo simu hii ni moja kati ya simu nyingi za Infinix zenye teknolojia ya Fast Charging hadi walt 10 kwa chaji.

Kwa upande wa upatikanaji simu hii kwa sasa inapatikana kwanza nchini India na inategemea kuzinduliwa kwenye nchi nyingine za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla miezi michache ijayo. Kama unataka kujua sifa kamili pamoja na bei ya Infinix Hot 9 soma hapa.

2 comments
  1. Habari. nimejaribu kutumia kwenye pc yangu ya window 10 lakini bado inagoma kuistall app naomb msaada wako tafadhari

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use