in

Majaribio ya Sehemu ya Group Chat Kupitia Tanzania Tech App

Sasa utaweza kuchat na watalamu wa teknolojia kupitia Tanzania Tech

Majaribio ya Sehemu ya Group Chat Kupitia Tanzania Tech App

Kama wewe ni mtumiaji wa app ya Tanzania Tech basi makala hii ni kwa ajili yako, na kama bado huja pakua app ya Tanzania Tech basi jaribu sasa app hii ili uweze kupata taarifa na mafunzo mbalimbali ya teknolojia kwa ukaribu zaidi na kwa haraka.

Kwa wale ambao tayari wanayo app ya Tanzania Tech na wanatumia toleo la zamani basi unaweza kupakua sasa toleo jipya ili kupata maboresho mapya pamoja na sehemu mpya ya “Group Chat”.

Majaribio ya Sehemu ya Group Chat Kupitia Tanzania Tech App

Kupitia sehemu hii utaweza kuchat na watalamu wa teknolojia wanaotumia programu ya Tanzania Tech kwa urahisi na haraka, kupitia sehemu hii una haja ya kujisajili kama tayari unayo akaunti ya Tanzania Tech ambayo ulisajili awali pale unapo tumia app ya Tanzania Tech. Kitu cha muhimu ni kuchagua (username) au jina ambalo itakuwa lina wakilisha akaunti yako kwenye sehemu ya kuchat.

Baada ya kuchagua (username) moja kwa moja unaweza kuchat na watu wote waliopo online kwa muda huo. Kama utakuwa haupo online, utaweza kuona meseji zilizopita muda mfupi uliopita na sio meseji zote, pia utaweza kuona meseji chache na sio meseji zote. Hii ni kwa sababu sehemu hii haifadhi data kwenye server kwa muda mrefu ili kulinda ubora na ufanyaji kazi wa haraka wa sehemu hiyo.

Majaribio ya Sehemu ya Group Chat Kupitia Tanzania Tech App

Sehemu hii ipo kwenye majaribio na bado tuna angalia njia bora ya kuboresha sehemu hii na kufanya iwe rahisi kutumia na iweze kuwa bora zaidi. Unaweza kupata sehemu hii ndani ya App ya Tanzania Tech kwa kubofya sehemu ya kuchat iliyopo kuju upande wa kulia. Kupitia hapo tutajifunza wote kwa pamoja jinsi ya kutumia sehemu hiyo ikiwa pamoja na matatizo mbalimbali ya teknolojia.

Hizi Hapa Apps Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu Yako ya Android

Kama umependa app ya Tanzania Tech unaweza kutupa nyota tano kupitia soko la Play Store, pia kama unataka kujua app zetu nyingine unaweza kuangalia app zetu nyingine hapa, au soma zaidi kuhusu app zetu hapa.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 4

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.