Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Simu hii inategemewa kuanzia kupatikana kuanzia tarehe 18 ya mwezi huu
Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Tayari tumesha angalia sifa na bei za Samsung Galaxy S20, S20 Plus pamoja na Galaxy S20 Ultra 5G na sasa hebu twende moja kwa moja tuka angalie sifa na bei za Samsung Galaxy Z Flip.

Kwa kuanza labda nikwambie kuwa Galaxy Z Flip ni tofauti kabisa na Galaxy Fold ambayo ilizinduliwa mwaka jana 2019, kwani najua watu wengi sana wanaweza kuchanganya simu hizi mbili kama matoleo yanayo fuatana. Kwa mujibu wa taarifa za awali tayari Samsung imeanza kushulikia simu mpya ya kujikunja ya Galaxy Fold 2 ambayo tunaweza kuiona baadae mwaka huu.

Advertisement

Baada ya kusema hayo sasa moja kwa moja twende tukangalie simu hii mpya ya Galaxy Z Flip. Tukianza na muonekano wa nje, Galaxy Z Flip imetengenezwa ikiwa ni simu ya kujikunja ambayo inajikunja kwa wima, tofauti na Galaxy Fold ambayo yenyewe inajikunja kwa upana. Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.7 ikiwa imefunuliwa kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED.

Kioo hicho cha ndani cha Galaxy Z Flip kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2636, huku ikiwa inasadiwa na teknolojia ya HDR10+ pamoja na Always-on display. Tukiwa bado kwa ndani simu hii inakuja na kamera ya selfie yenye uwezo wa hadi Megapixel 10, kamera ambayo ni wide lens ambayo pia ina uwezo wa kuchukua video za hadi 4K (2160p@30fps).

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Kwa nyuma au kwa nje simu hii inakuja na kioo kidogo cha inch 1.1 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, kioo hicho inakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 112 kwa 300. Kioo hicho nikigumu maana kinalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya Corning Gorilla Glass 6, mbali na hayo kioo hicho pia kinakuja na teknolojia ya Always-on display.

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Mbali ya kioo hicho, Galaxy Z Flip inakuja na kamera mbili kwa nyuma kamera kuu inakuja na Megapixel 12 ambayo hii ni wide lens huku kamera ya pili nayo ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni ultrawide lens. Kamera zote kwa ujumla zinaweza kuchukua video za hadi 4K, ambayo ni sawa na kusema simu hii inao uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 2160p@30/60fps. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED pamoja na teknolojia za HDR, na panorama.

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Sifa za Samsung Galaxy Z Flip

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 11080 x 2636 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.95 GHz Kryo 485 & 3×2.41 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SM8150 Snapdragon 855+ (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640 (700 MHz).
  • Ukubwa wa Ndani – GB 256 haina sehemu ya kuweka memory card.
  • Ukubwa wa RAM – GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 10 yenye f/2.4, 26mm (wide), 1.22µm, PDAF na uwezo wa video hadi 4K au 2160p@30/60fps, 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 12, yenye f/2.2, 12mm (ultrawide). Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za 4K na zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.2, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Mirror Black, Mirror Purple, na Mirror Gold.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja na eSIM (Nano-SIM, eSIM), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint Kwa pembeni kwenye kitufr cha kuwashia.

Bei ya Samsung Galaxy Z Flip

Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy Z Flip inategemewa kupatikana kuanzia terehe 18 mwezi huu kwa dollar za marekani $1,380 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za kitanzania 3,188,000 bila kodi. Simu hii inategemewa kuanza kupatikana kwanza kwa nchi za Marekani, Ulaya na Uingereza.

Kumbuka bei ya Galaxy Z Flip inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kupanda au kushuka kwa kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use