in

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M31

Zifahamu hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy M31

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M31

Baada ya kuvuma kwa tetesi siku kadhaa zilizopita, hivi leo Samsung imetangaza ujio wa simu mpya ya Galaxy M31 ambayo ni toleo la maboresho la simu mpya za Galaxy M30 pamoja na Galaxy M30s.

Kama ilivyo kwenye matoleo mengine yaliopita, simu hii mpya ya Galaxy M31 haina tofauti sana bali imeongezewa baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinafanya simu hii ibaki kuwa simu bora. Kwa upande wa kioo, Galaxy M31 inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED. Kioo hicho kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1080 x 2340, huku kikiwa na uwiano wa 19.5:9.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M31Kwenye kioo hicho kwa juu kuna kamera ya selfie ya Megapixel 32, kamera ambayo inauwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps, huku ikiwa imewezeshwa na teknolojia ya HDR.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 nyingine ikiwa na Megapixel 8 huku kamera mbili za mwisho zote zikiwa na Megapixel 5 kila moja. Kwa pamoja kamera hizo zinaweza kuchukua video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za hadi 2160p@30fps.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M31
Kwa upande wa sifa za ndani, Galaxy M31 inakuja na processor ya Exynos 9611 (10nm), ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128 GB na GB 64. Uhifadhi huo unaweza kuongezewa na Memory card ambayo inakaa kwenye sehemu ya kuweka Laini za simu. Sifa nyingine za Samsung Galaxy M31 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy M31

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400 pixels, pamoja na uwiano wa 19:9 ratio (~411 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9611 (10nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP3.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 64 yenye f/1.9, 1/3.1″, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 1/5″, 1.12µm, depth na nyingine inakuja na Megapixel 5 yenye f/2.2, 25mm (macro), 1/5.0″, 1.12µm na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 5 ambayo hii inakuja na f/2.2, (depth). Kamera zote zinauwzo wa kuchukua video za 4K
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 6000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Opal Black, Sapphire Blue, Pearl White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy M31

Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy M31 inategemewa kuanza kupatikana inchini India na inategemewa kuuzwa kwa rupee ya India Rs. 14,999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania TZS 484,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubalisha fedha pamoja na kodi.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M31
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.