Samsung Yazindua Simu Mpya ya Bei Rahisi ya Galaxy A01

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Samsung Galaxy A01
Samsung Yazindua Simu Mpya ya Bei Rahisi ya Galaxy A01 Samsung Yazindua Simu Mpya ya Bei Rahisi ya Galaxy A01

Kabla ya Samsung kuingiza sokoni simu zake mpya za daraja la juu za Samsung Galaxy S20, hapo jana kampuni hiyo imetangaza ujio wa simu yake mpya ya bei rahisi ya Galaxy A01. Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech, uta gundua kuwa simu hii ilitangazwa ujio wake toka mwaka 2019 mwezi November na hadi kufikia siku ya jana ndipo simu hii imetangazwa rasmi.

Samsung Yazindua Simu Mpya ya Bei Rahisi ya Galaxy A01

Kwa mujibu wa Samsung, simu hiyo mpya ya Galaxy A01 imezinduliwa jana huko nchini Vietnam na inakuja na kioo cha inch 5.7 kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya PLS TFT. Mbali na kioo, simu hii inakuja na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16.

Advertisement

Kwa upande wa processor Galaxy A01, inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 439 processor ambayo inakuja na uwezo wa CPU ya Octa-core (4×1.95 GHz Cortex-A53 & 4×1.45 GHz Cortex A53). Kama wewe ni mpenzi wa Game Galaxy A01 inakuja na GPU ya Adreno 505. Sifa nyingine na bei ya Galaxy A01 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A01

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 chenye teknolojia ya PLS TFT capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.95 GHz Cortex-A53 & 4×1.45 GHz Cortex A53)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM439 Snapdragon 439 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 505.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya microSDXC.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye f/2.2, 1/5″, 1.12µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13, yenye f/2.2, 28mm (wide), 1/3.1″, 1.12µm, AF na nyingine ikiwa na Megapixel 2, yenye f/2.4, 1.75µm, depth sensor camera. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Black, Blue, na Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer, proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Samsung Yazindua Simu Mpya ya Bei Rahisi ya Galaxy A01

Bei ya Samsung Galaxy A01

Kwa upande wa bei, Galaxy A01 inasemekana kuwa ni simu ya bei rahisi zaidi kutoka Samsung kwa mwaka huu, simu hii inategemewa kuuzwa kwa takribani Shilingi za kitanzania TZS 283,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka au kupungua kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use