Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu

Kusitishwa huku kunatokana na maambukizi ya virusi vya corona
Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu

Hatimaye mkutano mkubwa wa teknolojia MWC 2020 ambao hufanyika kila mwaka umetangazwa kusitishwa kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye tovuti ya GSM ambao ndio waandaji wa mkutano huo, kusitishwa kwa mkutano huo kumetokana na mlipuko wa virusi vya corona ambavyo vilianzia nchini China.

Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu

Mapema mwezi huu, kampuni mbalimbali za teknolojia zilitangaza kujitoa kushiriki mkutano huo kwa mwaka 2020 ikiwa ni hatua za kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi wa makampuni hayo. Mkutano wa MWC ni jukwaa maarufu ambalo hutumiwa na kampuni zote zinazo tengeneza simu duniani kuweza kuonyesha teknolojia mpya ambazo zinatarajiwa kuja kila mwaka.

Advertisement

Kampuni kama Samsung, mara nyingi imesha tumia mkutano huo kuzindua simu zake mpya kama Galaxy S7 ambayo ilizinduliwa kwenye mkutano huo mwaka 2016. Mbali na samsung zipo kampuni nyingi sana ambazo hutumia mkutano huo kutangaza bidhaa zake muhimu kila mwaka.

Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu

Kwa sasa virusi vya corona vinaonekana kuendelea kuathiri sekta mbalimbali za teknolojia nchini China ikiwa pamoja na duniani kwa ujumla, kwani mkutano huu hutumiwa na makampuni mengi hata yale yanayotoa huduma zake kwenye nchi za Afrika. Mwaka 2018 kampuni ya Tigo ilitumia mkutano huo kutangaza ushirikiano wake na Mastercard kwenye huduma yake ya Masterpass QR.

Kwa sasa China inaendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa homa ya corona kwa kuleta roboti maalum kwa ajili ya kusaidia kupambana na maambukizi mapya yanayotokana na virusi hivyo hatari.

Mkutano wa MWC 2020 Watangazwa Kusitishwa kwa Mwaka Huu

Hadi kufikia tarahe 10 Februari, idadi ya walioathirika na virusi hivyo nchini China ilikuwa imeongezeka hadi kufikia watu 40,171. Huku ikisemekana watu 28,942 wanahisiwa kuwa na virusi hivyo, lakini pia idadi ya wanao ruhusiwa kutoka Hospitali baada ya kupewa matibabu pia imeongezeka na kufikia watu 2651.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use