Kampuni ya Tecno inategemea kuanza mwaka 2020 kwa simu mpya ambayo inasamekana kuzinduliwa rasmi Februari 20. Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali mtandaoni, kampuni ya Tecno inatarajia kuzindua Tecno Camon 15 simu mpya inayosemekana kuja na teknolojia mpya ya kamera.
Mbali na kamera tetesi zinasema kuwa simu hiyo inatarajiwa kuja na muundo mpya kabisa huku pia ikiwa na aina mpya ya kioo ambacho kitakuwa na selfie kamera iliyopo juu ya kioo kama ilivyo simu mpya ya Infinix S5.
Pia inasemekana kuwa, Tecno Camon 15 itakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 665 tofauti na simu nyingi za Tecno ambazo zimetoka hivi karibuni. Simu hii pia itakuwa na uhifadhi wa ndani wa GB 32 huku ikiwezekana kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card ya hadi GB 256.
Kitu kingine cha tofauti kwenye simu hiyo inasemekana kuwa ni mfumo wa kamera, Tecno Camon 15 inatarajiwa kuja na kamera nne ambazo zipo kwenye mfumo mpya tofauti na simu nyingi za Tecno zilizotoka hivi karibuni, simu hiyo inatarajiwa kuja na kamera zenye uwezo wa Megapixel 48, Megapixel 8 huku nyingine mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 2 kila moja.
Kitu kikubwa kwenye kamera hizo inasemekana kuwa ni uwezo wa kamera hizo kupiga picha wakati wa usiku, hii ni kwa sababu hivi karibuni kupitia akaunti ya Twitter ya Tecno nchini India, imetoa tangazo la uzinduzi wa simu hiyo huku msemo wa uzinduzi wa simu hiyo ikiwa ni “Dark is Night” ikiwa na maana ya “Giza ni Usiku” hii ikiwa moja kwa moja ina ashiria kamera za simu hiyo.
Add light to your night and find out the bright side of the dark on 20th February! #StayTuned #NewYouWithCamon pic.twitter.com/IOID7oE4Ws
— TECNO Mobile India (@TecnoMobileInd) February 12, 2020
Mbali na hayo kwa sasa hakuna taarifa zaidi kuhusu simu hiyo, Kama unataka kujua zaidi kuhusu simu hii lini itafika Tanzania basi hakikisha unaendelea kutembelea Tovuti ya Tanzania Tech tutakupa taarifa kamili.