Kampuni ya Samsung ilizindua Galaxy M30 mwaka jana 2019, haiku ishia hapo mwezi September Samsung ilizindua Galaxy M30s, lakini kama haitoshi sasa jiandae na simu mpya ya Galaxy M31.
Kwa mujibu wa tovuti ya Samsung ya nchini India, simu hiyo mpya inatarajiwa kuzinduliwa nchini India siku ya jumanne ya tarehe 25 mwezi huu wa pili. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Galaxy M31 inategemea kuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na battery, kamera pamoja na kioo.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Galaxy M31 ni tofauti kabisa na Galaxy M30 na M30s kutokana na mtindo wake wa kamera ambao nadhani kwa sasa ni sawa kusema huo ndio mtindo wa kamera za simu za Samsung kuanzia mwaka huu 2020.
Kwa upande wa sifa, Galaxy M31 inasemekana kuja na battery kubwa ya mAh 6000 ambayo inaweza kudumu na chaji siku nzima kutoka na matumizi yako, pia simu hii inakuja na kioo cha sAMOLED ambacho kwa juu kinakuja na ukingo mdogo wa juu unao tumika kuhifadhi kamera ya mbele au selfie. Tukiongelea upande wa kamera, Galaxy M31 inaonekana kuja na kamera nne kwa nyuma, huku kamera moja kati ya hizo ikiwa na uwezo wa Megapixel 64.
Kwa upande wa processor inasemekana kuwa simu hii inaweza kuja na processor ya Snapdragon 665 SoC au processor ya Exynos 9611. Kwa sasa bado hakuna taarifa zenye uhakika kuhusu ilo. Kwa taarifa zaidi kuhusu simu hii, ikiwa pamoja na kujua sifa na bei yake kamili hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.