Kampuni ya Sony kupitia mkutano wa CES 2020, imetangaza ujio wa kifaa kipya cha Game cha PlayStation 5 (PS5). Kwa mujibu wa Sony, kifaa hicho kipya kinategemewa kuja na sifa bora zaidi kuliko kifaa cha PS4 ambacho kilitoka mwaka uliopita.
Kupitia mkutano huo, Sony ilitangaza Logo mpya ya PS5 ambayo ndio itakuwu inatumika kwenye kifaa hicho pamoja na baadhi ya sifa za kifaa hicho kama vile uwezo wa 3D audio support pamoja na hard disk ya SSD (solid-state drive) ambayo inategemewa kufanya PS5 kusoma Game mbalimbali kwa haraka. Pia inasemekana PS5 itakuwa na uwezo wa 8K graphics.
Kwa upande wa sifa za ndani, PS5 inasemekana itakuja na eight-core CPU ( ambayo itakuwa ni AMD Zen 2 architecture), pamoja na GPU kutoka AMD Radeon Navi hardware. Mbali na hayo pia inasemekana PlayStation 5 itakuja na viendesheo (Controllerz) bora zaidi.
Japo kuwa kupitia mkutano huo wa CES 2020, Sony haikuonyesha muonekano wa PlayStation 5, lakini kwa mujibu wa tovuti ya CNN Business, PS5 inategemea kuwa na muonekano wa kipekee ambao unakuja na alama ya V katikati ambayo inasemekana ina maana namba 5 kwa lugha ya kirumi.
Kuhusu upatikanaji, kwa habari zilizopo sasa PlayStation 5 inatarajiwa kutoka mwezi wa sita (June) mwaka huu 2020 kupitia kwenye mkutano wa E3 expo (2020), mkutano ambao unategemewa kufanyika huko Los Angeles, nchini Marekani. Kuhakikisha kuwa hupitwi na uzinduzi huu, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
jamaninawapendawote