Jiandae na Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Hivi Karibuni

Simu ya kwanza ya infinix yenye kamera inayojificha kwa juu (Pop-up selfie)
Jiandae na Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Hivi Karibuni Jiandae na Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Hivi Karibuni

Kampuni ya Infinix inategemea kuanza mwaka 2020 na matoleo mapya ya simu zake ambazo zina semekana kuja na mtindo mpya na wakisasa. Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali mtandaoni, infinix inategemea kuanza na toleo la simu mpya ya Infinix S5 Pro ambayo inasemekana kuja na mtindo wa kisasa pamoja na teknolojia mpya ya kamera ya mbele au selfie.

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Hivi Karibuni

Kwa mujibu wa tovuti ya Gizmochina, Simu hiyo mpya ya Infinix S5 Pro inasemekana kuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 18 mwezi February huku ikija na teknolojia mpya mbalimbali ambazo hazikwepo awali kwenye simu za Infinix. Moja ya teknolojia hiyo ni Pop-up Selfie kamera ambayo hii hufanya kioo cha simu hiyo kuwa kikubwa zaidi kisicho na kingo kubwa kutokana na kamera ya mbele kujificha juu ya simu hiyo.

Advertisement

https://gfycat.com/basicsatisfiedblacklemur

Inasemekana kuwa, simu hiyo itakuja na battery kubwa ya 4,000mAh battery ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi, pia simu hii inategemea kuwa na mfumo wa AI ambao utakuwa unawezeshwa na processor mpya za MediaTek SoC. Pia inasemekana kuwa simu hii itakuja na aina mpya ya fingerprint ambayo itakuwa kwa mbele tofauti na simu za Infinix S5 zilizo zinduliwa mwaka 2019.

Kwa sasa hayo ndio machache ambayo tumefanikiwa kufahamu kuhusu simu hiyo mpya ya Infinix S5 Pro. Kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use