Kampuni ya Infinix inategemea kuanza mwaka 2020 na matoleo mapya ya simu zake ambazo zina semekana kuja na mtindo mpya na wakisasa. Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali mtandaoni, infinix inategemea kuanza na toleo la simu mpya ya Infinix S5 Pro ambayo inasemekana kuja na mtindo wa kisasa pamoja na teknolojia mpya ya kamera ya mbele au selfie.
Kwa mujibu wa tovuti ya Gizmochina, Simu hiyo mpya ya Infinix S5 Pro inasemekana kuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 18 mwezi February huku ikija na teknolojia mpya mbalimbali ambazo hazikwepo awali kwenye simu za Infinix. Moja ya teknolojia hiyo ni Pop-up Selfie kamera ambayo hii hufanya kioo cha simu hiyo kuwa kikubwa zaidi kisicho na kingo kubwa kutokana na kamera ya mbele kujificha juu ya simu hiyo.
https://gfycat.com/basicsatisfiedblacklemur
Inasemekana kuwa, simu hiyo itakuja na battery kubwa ya 4,000mAh battery ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi, pia simu hii inategemea kuwa na mfumo wa AI ambao utakuwa unawezeshwa na processor mpya za MediaTek SoC. Pia inasemekana kuwa simu hii itakuja na aina mpya ya fingerprint ambayo itakuwa kwa mbele tofauti na simu za Infinix S5 zilizo zinduliwa mwaka 2019.
Kwa sasa hayo ndio machache ambayo tumefanikiwa kufahamu kuhusu simu hiyo mpya ya Infinix S5 Pro. Kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.