Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite

Simu hii ni bora kwa upande wa kamera kuliko hata Galaxy S10 yenyewe
Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech na Price in Tanzania, basi lazima unajua hivi karibuni Samsung imezindua rasmi simu yake mpya ya Galaxy S10 Lite. Simu hii inakuja na sifa bora na tofauti kabisa na simu ya Galaxy S10 ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka 2019.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha sifa za simu hii ikiwa pamoja na kwa nini nakwambia simu hii inakuja na sifa bora pengine kuliko Galaxy S10 yenyewe, basi bila kupoteza muda twende tukaangalie sifa za Samsung Galaxy S10 Lite.

Advertisement

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite

Sifa za Samsung Galaxy S10 Lite

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SM8150 Snapdragon 855 (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6 au GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 MP, f/2.0, 26mm (wide), 1/2.0″, 0.8µm, PDAF, Super Steady OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 12 MP, f/2.2, 12mm (ultrawide), kamera ya mwisho ni Megapixel 5 MP, f/2.4, 1/5.0″, 1.12µm, dedicated macro camera. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Prism White, Prism Black, Prism Blue.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint (under display, optical), accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite

Bei ya Samsung Galaxy S10 Lite

Kwa upande wa bei ya Samsung Galaxy S10 Lite, kwa mujibu wa samsung simu hii inatarajiwa kuingia sokoni mwezi huu na inategemewa kupatikana kwa €650 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 1,668,000 bila kodi. Bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha. Unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili za simu hii pamoja na bei.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use