Sasa ni Lazima Kuandika Tarehe ya Kuzaliwa Ili Kujiunga na Instagram

Tarehe hiyo itakuwa haionekani na mtu yoyote isipokuwa wewe
Sasa ni Lazima Kuandika Tarehe ya Kuzaliwa Ili Kujiunga na Instagram Sasa ni Lazima Kuandika Tarehe ya Kuzaliwa Ili Kujiunga na Instagram

Hivi karibuni instagram imetangaza kuja na mabadiliko kadhaa, moja ya mabadiliko hayo ni pamoja na sehemu mpya ya tarehe ya kuzaliwa ambayo ni lazima kuijaza ili kujiunga na mtandao huo.

Kwa mujibu wa Instagram, kwa sasa kila mtu atakayetaka kujiunga na mtandao huo analazimika kuandika tarehe yake alisi ya kuzaliwa. Kwa mujibu wa blog ya Instagram, uamuzi wa kueleta sehemu ya kujaza tarehe ya kuzaliwa kabla ya kujiunga na mtandao huo imekuja kwa lengo la kuzuia watoto chini ya umri wa miaka 13 kutumia mtandao huo.

Sasa ni Lazima Kuandika Tarehe ya Kuzaliwa Ili Kujiunga na Instagram

Advertisement

Hata hivyo Instagram imeainisha kuwa, kwa wale ambao tayari wanazo profile za Instagram tarehe ya kuzaliwa iliyopo kwenye kurasa ya facebook iliyo unganishwa na instagram ndio itatumika kwenye akaunti ya Instagram. Kwa hiyo kama ukibadilisha tarehe ya kuzaliwa kwenye ukurasa wako wa facebook moja kwa moja tarehe hiyo pia itabadilika kwenye akaunti yako ya Instagram.

Vilevile kama huja unganisha akaunti yako ya Instagram na ukurasa wako wa Facebook basi utatakiwa kuweka tarehe yako kamili ya kuzaliwa kupitia Settings kwenye akaunti yako ya Instagram. Kwa mujibu wa instagram, tarehe hiyo haitokuwa inaonekana na mtu yoyote sipokuwa wewe mwenyewe.

Mbali na hayo sehemu nyingine ambayo imeongezwa kwenye mtandao huo ni pamoja na sehemu mpya ya kuweza kuchagua ni nani anaweza kutuma DM. Kupitia sehemu hiyo mpya mtumiaji anaweza kuchagua watu aliowafuata pekee ndio waweze kutuma DM pamoja na kuwa na uwezo wa kuwekwa kwenye group na watu hao pekee.

Sasa ni Lazima Kuandika Tarehe ya Kuzaliwa Ili Kujiunga na Instagram

Kama mtumiaji akiwasha sehemu hii hatoweza kuendelea kupokea DM au Direct Message kutoka kwa watu wengine isipokuwa tu watu ambao amewafuata au ame wa-follow. Sehemu hizi zote zinatagemewa kuwafikiwa watu wote siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use