Kama ilivyokuwa kwa Tecno, kampuni ya Infinix kwa mwaka 2019 nayo imekuja na simu mpya ambazo ni bora zenye muonekano mzuri pamoja na sifa bora, mbali ya yote simu hizi zinakuja zikiwa zinauzwa kwa bei rahisi ukilinganisha na uzuri na sifa za simu hizo.
Kama ukiangalia list ya simu za infinix utaweza kugundua kuwa kampuni ya Infinix imefanya mabadiliko makubwa ya simu zake kuanzia muonekano, sifa na hata bei ya simu hizo imezidi kuwa nafuu ukilinganisha na muonekano na sifa za simu hizo
Kupitia makala hii nitaenda kukujulisha simu zote mpya za infinix zilizotoka kwa mwaka 2019, ikiwa pamoja na maelezo mafupi kuhusu simu hizo, kama unataka kupata maelezo zaidi basi unaweza kubofya sehemu ya Soma zaidi iliyopo chini ya kila simu kwenye list hii. Kumbuka pia simu zote kwenye list hii tayari zinapatikana kupitia maduka mbalimbali hapa nchini Tanzania.
TABLE OF CONTENTS
Infinix Hot 7 – January 2019
Infinix Hot 7 ni toleo bora la simu za infinix, simu hii inakuja na muonekano mzuri pamoja na sifa ambazo zinafanana na thamani ya pesa unayo nunulia simu hii. Mbali ya yote kamera za simu hii ni bora na zenye uwezo wa kuchukua picha nzuri sana ukilinganisha na simu nyingi za infinix ambazo zimetoka miaka iliyopita. Unaweza kuipata Infinix Hot 7 kwa bei kuanzia TZS 260,000 hadi TZS 320,000 bei inaweza kutofautiana kulingana na eneo.
Infinix Zero 6 – March 2019
Kama kweli wewe ni mpenzi wa simu zenye kamera nzuri basi lazima utakuwa umewahi kusikia simu ya Infinix Zero 6, simu hii inakuja na kamera nzuri sana na pia inakuja na sifa bora zaidi ambazo zinafanana na bei yake. Kifupi ni kuwa, kweli kampuni ya infinix imekuwa ikijitahidi sana kuja na simu zenye ubora pamoja na kamera nzuri kama watu wengi wanavyopenda. Simu hii inakuja kwa matoleo mawili ya Infinix Zero 6 pamoja na Zero 6 Pro. Unaweza kupata simu hii kuanzia TZS 600,000 had TZS 850,000, kumbuka bei inaweza kubadlika.
Infinix S4 – April 2019
Kwa wale wapenzi wa kamera hasa selfie basi na uhakika tayari wanajua kuhusu infinix S4, simu hii ni toleo la maboresho la infinix S3 ambayo ilitoka mwaka uliopita, simu hii kwa sasa inakuja na sifa nzuri sana pamoja na muonekano wa kisasa hasa kwenye kioo chale kutokana na muundo wake wa water drop notch, simu hii inakuja na kamera zenye nguvu sana huku kamera ya mbele ikiwa na MP 32. Unaweza kupata Infinix S4 kwa matoleo mawili ya S4 na S4 Pro, Kwa upande wa bei unaweza kupata simu hii kuanzia TZS 350,000 hadi TZS 450,000.
Infinix Smart 3 – June 2019
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda simu zenye uwezo mzuri lakini kwa bei nafuu basi ni vyema ufahamu simu mpya ya Infinix Smart 3, simu hizi zinakuja na matoleo mawili toleo la Smart 3 pamoja na Smart 3 Plus. Simu hii inakuja na uwezo mzuri wa kudumu na chaji ikiwa pamoja na kupiga picha nzuri sana ambazo unaweza kuzifanya ziwe nzuri zaidi kwa kutumia mfumo wa AI ambao upo ndani ya simu hizo. Unaweza kupata Smart 3 au Smart 3 Plus kuanzia TZS 370,000 hadi TZS 420,000.
Infinix Note 6 – July 2019
Infinix Note 6 ni moja kati ya simu bora ambazo naweza kusema inashindania na pacha mwenzake TECNO Phantom 9, simu hii inakuja na sifa nzuri pamoja na muonekano wa kisasa huku nayo ikiwa na kioo kizuri na bora cha AMOLED. Mbali na ubora wake kwa upande wa sifa simu hii pia inakuja na kamer nzuri ikiwa pamoja na battery bora yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi. Unaweza kupata Infinix Note 6 kuanzia TZS 550,000 hadi TZS 670,000.
Infinix Hot 8 – September 2019
Kwa mara nyingine wapenzi wa simu za bei rahisi zenye ubora wanapatiwa toleo jipya la Infinix Hot 8, simu hii ni moja kati ya simu ambazo zinapatikana kwenye list ya simu zinazopendwa zaidi na watumiaji wa Infinix, huku ikiwa inapatikana kwa bei nafuu zaidi. Simu hii inakuja na kamera bora ikiwa na teknolojia ya AI pamoja na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji kwa muda mrefu. Infinix Hot 8 inapatikana Tanzania kwa TZS 280,000 hadi TZS 380,000. Bei inaweza kuwa tofauti kutokana na eneo ulilopo kwa sasa.
Infinix S5 – October 2019
Kampuni ya Infinix imefunga mwaka 2019 kwa kutoa simu mpya ya Infinix S5, simu hii ni moja kati ya simu nzuri sana kwa wapenzi wa picha na pia kwa wale wanaotaka kwenda na wakati. Kama unataka simu yenye muonekano mzuri na yenye sifa bora basi simu hii ndio simu yako kwa sasa. Kupitia simu hii utaweza kupata mfumo mpya wa Android 9 wenye sehemu mpya mbalimbali ikiwa pamoja na sehemu itakayo kuwezesha kupokea simu yako bila kuishika. Unaweza kuipata Infinix S5 kwa TZS 350,000 had TZS 400,000. Bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo.
Na hizo ndio simu zote mpya za Infinix zilizotoka mwaka 2019, kama unataka kujua simu nyingine bora za Infinix za kununua kwa sasa hakikisha unasoma hapa kujua simu nzuri za infinix ambazo unaweza kuzipata kwa bei chini ya TZS 300,000. Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.