Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

Utaweza kupata beat ya nyimbo yoyote ile unayoita kwa haraka zaidi
Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat) Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

Kama wewe ni mtaalamu wa muziki basi inaweza kuwa hii sio makala sahihi kwako kwani ukweli ni kwamba binafsi sina ujuzi wa muziki hivyo inawezekana kuwa njia hizi zikawa sio bora kama njia ambayo unaijua wewe. Lakini kwa wenzangu na mimi ambao hatujui mambo ya sound engineer basi pengine makala hii inaweza kuwa msaada kwako.

Kupitia makala hii nitaenda kukuonyesha njia rahisi ambazo unaweza kutumia kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote na kubakia na beat pekee, njia hizi ni rahisi sana kutumia na kwa baadhi ya njia huna haja ya kuwa na programu yoyote ili kuweza kufanikisha hili, unahitaji internet pamoja na uwezo wa ku-upload nyimbo mtandaoni pamoja na kuipakuwa baada ya kufanikiwa kuondoa maneno kwenye nyimbo husika. Basi bila kupoteza muda twende tuka angalie njia hizi.

https://www.youtube.com/watch?v=fNaRDximF48

Advertisement

Njia ya Kwanza

Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

X-minus pro ni tovuti ambayo inaweza kukusaidia kuweza kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote kwa haraka zaidi, tovuti hii ni rahisi kutumia na kwa maoni yangu inaweza kutoa maneno kwenye beat kwa kiwango kikubwa sana, unaweza kusikia mfano hapo chini.

Unaweza kutembelea tovuti hiyo na kujaribu kutoa maneno kwenye nyimbo yoyote, unachotakiwa kufanya ni kubofya kutufe cha select File kisha upload nyimbo na baada ya kapo anza kusikiliza nyimbo hiyo kama maneno yameondolewa vizuri, kama bado unaweza kucheza na sehemu ya chini ambapo unaweza kurekebisha jinsi nyimbo inavyo sikika.

Tembela Tovuti Hapa

Njia ya Pili

Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

Audio alter ni tovuti nyingine ambayo inakusaidia sana kuweza kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote, tofauti na tovuti iliyopita tovuti hii ni rahisi zaidi kutumia kwani huna haja ya kufanya chochote zaidi ya ku-upload nyimbo kisha ikimaliza una download tena ikiwa imeondolewa maneno. Tovuti hii nayo pia inajitahidi kuweza kuondoa maneno kwenye nyimbo unaweza kusikia mfano hapo chini.

Unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hiyo na kubofya kitufe cha browse na kisha chagua nyimbo unayotaka kisha bofya submit baada ya hapo nyimbo ita upload na ikimaliza hapo hapo utaruhusiwa kupakua nyimbo ambayo tayari imetolewa maneno.

Tembela Tovuti Hapa

Njia ya Tatu

Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

Tovuti ya mwisho kwenye list hii inaitwa Vocal removal, tovuti hii haina tofauti na tovuti nyingine kwenye list hii lakini yenyewe hii kama ilivyo tovuti ya kwanza inakupa uwezo wa kubadilisha jinsi nyimbo inavyo sikika kwa kutumia sehemu za kuedit zilizopo kwa chini ya nyimbo baada ya ku-upload. Unaweza kusikiliza mfano wa nyimbo iliyo ondolewa maneno kwa kutumia tovuti hii.

Kutumia tovuti hii ni rahisa sana tembelea tovuti hiyo kisha bofya Browse my files kisha endelea kwa kuchagua nyimbo unayoitaka kisha endelea kwa kusikiliza nyimbo kama umependa jinsi inavyo imba basi bofya kitufe cha Save kupakua nyimbo iliyo ondolewa maneno.

Tembela Tovuti Hapa

Njia ya Nne

Jinsi ya Kuondoa Maneno Kwenye Nyimbo Yoyote (Baki na Beat)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki kompyuta basi njia hii inaweza kuwa njia bora zaidi kati ya njia zote hizi, unachotakiwa kufanya ni kutembelea kupakua programu ya Adobe audition, kama huna programu hiyo basi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata programu hiyo bure kabisa bila kulipia kwa kompyuta za Windows. Baada ya kupakua programu hiyo basi fungua programu hiyo kisha File > Open kisha chagua nyimbo unayora kuondoa maneno.

Baada ya hapo bofya sehemu ya Effect > Stereo Imagery > Center channel Extractor kisha kwenye sehemu ya preset chagua sehemu ya Vocal removal bofya hapo kisha Apply na moja kwa moja Play nyimbo na utasikia ikiwa imeondolewa maneno. Unaweza kusikia mfano hapo chini.

Na hizo ndio njia ambazo unaweza kutumia kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote kwa haraka zaidi. Kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapa chini. Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya YouTube hapa kwani huwa tunajifunza zaidi kwa vitendo.

2 comments
    1. samahani naomba kujua namna ya kutumia tanzania tech maan nimeshindwa kutoa maneno kwenye nyimbo na kubaki na beat

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use