Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55

TV hii inaingia kwenye historia kwa kuwa TV ya kwanza kabisa kutoka Nokia
Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55 Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55

Siku chache baada ya tetesi kuhusu kampuni ya Nokia kujiungiza kwenye biashara ya TV, hivi leo kampuni hiyo imetangaza wazi kuingia kwenye biashara hiyo na kutambulisha TV yake ya kwanza ya Nokia 139 cm.

Nokia 139 cm ni Smart TV mpya kabisa kutoka Nokia na inakuja ikiwa na muonekano mzuri sana pengine tofauti na ambavyo wengi walifikiria. TV hii inakuja na kioo chenye ukubwa wa sentimita 139 ambayo ni sawa na Inch 55 pamoja na resolution ya Ultra HD (4K), 3840 x 2160 pixel, vilevile TV hii inakuja ikiwa inaendeshwa na mfumo wa Android 9 TV mfumo ambao unakuja na soko la Play Store moja kwa moja ndani ya TV hiyo.

Advertisement

Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55

Mbali ya hayo Smart TV hii mpya kutoka Nokia ina endeshwa na processor ya PureX quad-core processor yenye speed ya hadi Ghz 1, huku ikisaidiwa na RAM ya hadi GB 2.25 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 16. Vilevile Smart TV Nokia 139 cm inakuja na GPU ya Mali 450 MP4.

Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55

Kwa upande wa sauti, TV hii ya Nokia inakuja na teknolojia mbalimbali kama vile mfumo wa spika za ndani zenye Walt 24 zilizo tengenezwa na JBL, mfumo wa Dolby Audio, pamoja na DTS Trusurround. Vilevile TV hii inakuja ikiwa inauwezo wa kucheza format za sauti za MP3, WMA, M4A, AAC, MP2, PCM, pamoja na MPEG.

Hatimaye Nokia Yazindua Nokia 139 cm Smart TV ya Inch-55

Kwa upande wa Picha TV hii ya Nokia inakuja ikiwa ina uwezo wa kuonyesha picha angavu za hadi 4K, huku ikiwa na uwezo wa kutumia Flash kucheza picha jongefu (Video) za format mbalimbali za MPG, AVI, TS, MOV, MKV, DAT, MP4, VOB, RM, pamoja na RMVB. Mbali na hayo TV hii inakuja na mfumo wa WiFi pamoja na sehemu mbili za kuchomeka USB Flash na sehemu tatu za kuchomeka waya au kifaa chochote kinachotumia HDMI.

Bei ya Nokia Smart TV

Kwa upande wa bei ya Nokia Smart TV, kwa mujibu wa Flipkart TV hii inatarajiwa kuuzwa kwanza kwa nchini India kuanzia tarehe 10 mwezi huu kwa Rupee Rs. 41,999 ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania TZS 1,354,000 bila kodi. Kumbuka TV hii itakapofika hapa Tanzania bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi pamoja na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use