in

Samsung Galaxy S11 Kuja na Kamera Kubwa ya Megapixel 108

Simu hii inasemekana kuzinduliwa mwezi wa pili mwaka 2020

Samsung Galaxy S11 Kuja na Kamera Kubwa ya Megapixel 108

Ikiwa imebaki miezi michache hadi kufika mwezi wa pili mwaka 2020, mwezi ambao ndio unao tegemewa na wengi kuona teknolojia mpya zitakazoletwa na simu mpya za Samsung Galaxy 11, huku mtandaoni tayari tetesi zimeanza kuibuka kuhusu kamera za simu hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Galaxy S11 inasemekana kuwa itakuja na kamera zaidi ya moja kwa nyuma, na moja ya kamera hiyo inategemewa kuwa na uwezo wa hadi Megapixel 108. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika @UniverseIce kutoka twitter, Simu hiyo inategemewa kuwa na sensor hiyo ambayo itakuwa ni mpya kabisa kutoka Samsung na sio kama ile inayotumika kwenye Xiaomi Mi CC9 Pro iliyo zinduliwa rasmi siku ya leo mda mchache uliopita

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mbali na hayo inasemekana kuwa simu hiyo itakuja na kioo cha kisasa chenye refresh rate hadi 90Hz kioo ambacho pia kitakuwa na kamera ya mbele ya kisasa ambayo ipo juu ya kioo. Kwa sasa bado haijajulika kamera hiyo ya mbele itakuwa na uwezo gani, lakini tuendelee kusubiri pengine siku sio nyingi tutasikia tetesi nyingine kuhusu hilo.

Samsung Galaxy S11 Kuja na Kamera Kubwa ya Megapixel 108

Tetesi nyingine ambazo zina sambaa mtandaoni ni pamoja na kuwa simu hiyo itakuja na mtandao wa 5G kwa simu zote, ikiwa pamoja na uwezo wa RAM hadi GB 12. Pia inasemekana kuwa simu hiyo inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa kati ya GB 512 hadi GB 128 pamoja na memory card ya hadi TB 1.

Kwa sasa hayo ndio machache yanayohusu simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy S11, kama unataka kujua zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kwa sasa kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma sifa kamili za Samsung Galaxy S10 hapa.

Samsung Galaxy S11 Kuja na Kamera Kubwa ya Megapixel 108
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.