Kampuni ya Motorola nayo imeingia rasmi kwenye ulimwengu wa simu zinazo jikunja (Foldable Phone), hapo jana kampuni hiyo imezindua simu yake mpya ya Motorola Razr (2019) ambayo ni simu yenye muonekano kama simu ya zamani ya Motorola Razr ambayo ilikuwa ni simu bora sana kwenye miaka ya 90 kama wewe ni muhenga basi lazima unaijua simu hii.
Tofauti na ambayo simu za kujikunja za samsung na Huawei zilivyo, Motorola Razr (2019) ni simu ya kwa kuja na mtindo wa aina hii wa kujikunja kwa juu huku simu hiyo ikiwa inakuja na mtindo wa simu ya kawaida tofauti na simu nyingine za kujikunja ambazo hizo huwa tablet pale unapozikunjua.
Simu hii mpya ya Motorola Razr (2019) inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya pOLED au Plastic OLED ambacho kina kuja na mtindo wa kujikunja, kwa nyuma simu hii inakuja na kioo cha inch 2.7 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED. Kioo hicho cha nyuma kime tengenezwa kwa glass tofauti na kioo cha ndani ambacho ni plastiki.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu (Picha kutoka CNET), kioo hicho cha nje kinaweza kutumika kufanya vitu mbalimbali kama vile kuendesha music player, kusoma meseji, kupiga picha simu hiyo ikiwa imefungwa pamoja uwezo wa kuendesha baadhi ya apps na mambo mengine mbalimbali.
Kioo cha ndani kinakuja na resolution ya 2142 x 876 pixels huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya milioni 16. Juu ya kioo cha ndani kuna ukingo wa juu wenye spika pamoja na kamera ya Megapixel 5 ambayo inauwezo wa kuchukua video za hadi 1080p. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 16 ambayo inauwezo wa kuchukua video hadi za 4K, kamera hii pia inaweza kuwa kamera ya nyuma na kuwa Selfie pale unapofunika simu hiyo.
Kwa upande mwingine wa sifa Motorola Razr (2019) sio simu yenye uwezo mkubwa sana kama ambavyo unatarajia, simu hii inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 128. Simu hii haina sehemu ya kuweka memory card hivyo kama GB 128 haikutoshi pengine simu hii sio chaguo bora kwako.
Motorola Razr (2019) pia haina sehemu ya kuchomeka headphone na pia haina radio kwa wale wapenzi wa radio. Kama unataka kusikiliza muziki kupitia earphone za pini, basi utaweza kutumia waya maalum ambao unakuja ndani ya box. Sifa nyingine za Motorola Razr (2019) ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Motorola Razr (2019)
Utangulizi
- Model – Motorola Razr (2019)
- Imetangazwa – 2019, November
- Itazinduliwa – 2019, December
- Upatikanaji – 2020, January
Muundo
- Vipimo – Unfolded 172 x 72 x 6.9mm / Folded 94 x 72 x 14mm
- Uzito – 205g (7.2 oz)
- Rangi – Nyeusi
Mtandao
- Uwezo wa 2G – Ndio
- Uwezo wa 3G – Ndio
- Uwezo wa 4G – Ndio
- Aina ya laini – Nano SIM
- Idadi ya laini – Laini Mbili ikiwa na eSIM
Kioo
- Aina ya kioo – OLED
- Ukubwa – inch 6.2
- Uwiano – 2142 x 876 pixels
- Idadi ya pixel – 373 ppi density
- Ulinzi – Corning Gorilla Glass
- Secondary Display – 2.7-inch glass OLED, 800 x 600 pixels (4:3)
Media
- FM Radio – Haina Radio
- Earphone Jack – Haina sehemu ya kuchomeka headphone
Kamera
- Idadi ya Kamera – Kamera Moja ya Mbele
- Kamera kuu – 16 MP, f/1.7, PDAF
- Video – 2160p@30fps, 1080p@30fps
- Flash – LED flash
- Idadi ya selfie – Single Camera
- Selfie kamera – Unfolded 5 MP / Folded 16 MP
- Video – Unfolded 720p@30fps / Folded 2160p@30fps, 1080p@30fps
Mfumo Endeshaji
- OS – Android 9.0 (Pie)
- Mfumo wa simu – Android One
Sifa za Ndani
- Chipset – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (10 nm)
- CPU – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver)
- GPU – Adreno 616
- RAM – 6 GB
- Uhifadhi wa Ndani – 128 GB
- Memory kadi – Haina Memory card
- Sensors – Fingerprint (front-mounted), accelerometer, proximity, compass
Viunganishi
- Bluetooth – 5.0, A2DP, LE
- Wi-fi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, Wi-Fi Direct
- Wi-fi Hotspot – Ndio
- USB – 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
- GPS – Yes, with A-GPS, GLONASS, BDS
- NFC – Ndio
Battery
- Aina ya Battery – Li-Poly (Lithium Polymer)
- Uwezo – 2510 mAh battery
- Muundo – Battery isiyotoka
Bei ya Motorola Razr (2019)
Kwa upande wa bei Motorola Razr (2019) sio simu ya bei rahisi sana japokuwa kwangu naona kama inakuja na sifa za kawaida kwa simu ya mtindo huu. Kwa mujibu wa Motorola, simu hii inategemea kuanza kupatikana kuanzia mwezi wa kwanza mwaka 2020 na watu wanaweza kuanza kutoa oda ya simu hii kuanzia mwezi Disemba mwaka huu 2019.
Motorola Razr (2019) inategemea kuanza kupatikana kwa nchini Marekani chini ya mtandao wa simu wa Verizon kwa dollar za marekani $1,500 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 3,463,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.