Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Fahamu kwanini ni muhimu sana kuzima na kuwasha simu yako
Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Ni wazi kuwa smartphone zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku kiasi kwamba pale simu yako inapokuwa imezima angalau kwa dakika chache unakuwa na wasiwasi wa kushindwa kufanya mambo yako ya kila siku.

Lakini ni kweli kwamba “kila kitu huchoka” nahisi hii ni sababu ya wewe kuendelea kusoma makala hii kama unataka kujua kwanini ni muhimu ku-restart au kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa wiki.

Advertisement

Pia kupitia makala hii nitakueleza ni kwanini ni muhimu kufanya hivyo hasa pale simu yako inapokuwa na matatizo mbalimbali ambayo nitakutajia kwenye makala hii, basi bila kupoteza muda twende kwenye sababu ya kwanza kabisa.

Husaidia Simu Kufanya Kazi Haraka

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia programu nyingi kwenye simu yako na ungependa simu yako iwe inafanya kazi kwa haraka zaidi basi ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa siku au ukishindwa sana angalau mara moja kwa wiki.

Hii husaidia baadhi ya programu unazo tumia kuacha kutumia kiasi kIkubwa cha RAM mpaka hapo utakapofungua tena. Kama ulikuwa hujui, mara nyingi smartphone huwa na mtindo wa kutofunga programu kabisa na badala yake huifadhiwa programu husika kwenye memory (RAM) ili wakati mwingine unapo fungua programu hiyo iweze kufunguka kwa haraka.

Mara nyingi kama umefungua programu nyingi kwa kipindi kirefu basi zote huwekwa kwenye memory na kufanya simu yako ichukue kiasi kikubwa cha RAM.

Kuzima na kuwasha simu yako husaidia programu hizo kufutwa kwenye memory (RAM) hadi hapo utakapofungua programu hizo kwa mara nyingine, hivyo ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa wiki au mara moja kwa siku hasa kama unatumia programu nyingi kwenye simu yako.

Huasaidia Programu Kama WhatsApp, Instagram na Facebook

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Kama umekuwa ukikutana na matatizo mengi ya kushindwa kutumia programu yako ya WhatsApp, Instagram na Facebook basi ni wakati wa kujaribu kuzima na kuwasha simu yako. Programu hizo zinajulikana kwa kutumia kiasi kikubwa cha memory (RAM) kwenye simu yako hii ndio maana ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako hasa unapokuwa unaona matatizo mengi kwenye App moja kati ya hizo.

Pia vile vile unaweza kujaribu kuondoa cache ya programu hizo kwani programu hizi zinakuja na mtindo ambao unawezesha programu hizo kuendelea kuwa na kumbukumbu ya matumizi yako kwa kipindi cha muda maalum, unaweza kuondoa cache kwenye moja kati ya programu hizo kwa kufuata hatua hizi.

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Ingia kwenye Settings > Apps > “Chagua App unayotaka” > Storage > Clear Cache. Kumbukwa kwa kufanya hivi itakubidi kuingia tena kwenye akaunti zako kwa njia hii itaondoa data zote zilizo hifadhiwa kwenye simu yako. Kama unatumia simu za iPhone unaweza kufuata hatua hizo hapo chini.

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Ingia kwenye Settings > iPhone Storage > “Subiri App zote zionekane kisha chagua app unayoitaka” > Offload App. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kuondoa Cache kwenye app hizo za instagram, Facebook na WhatsApp.

Husaidia Simu Kudumu na Chaji

Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki

Kama simu yako imekuwa na mtindo wa kuisha chaji haraka kuliko kawaida basi moja ya sababu ni hii ya kutokuzima kabisa simu yako. Hii husababishwa na jambo lile lile ambalo tumekua tukiongelea tokea mwanzo wa mada hii.

Mara nyingi app huifadhiwa kwenye RAM hata baada ya wewe kuacha kuzitumia, sasa hii husababisha simu yako kutumia kiasi kikubwa cha chaji kuweza kuendasha RAM ya simu yako ili kusaidia programu hizo kuendelea kuweko kwenye RAM.

Hii ni kwasababu mara nyingi RAM inatumia kiasi kikubwa cha umeme unao zalishwa na battery ya simu yako pale unapofungua programu nyingi kwa wakati mmoja, hapa kwa wale wapenzi wa game tunaelewana kwani nadhani mnajua kuwa kadri game inavyo onyesha vizuri zaidi ndio simu yako inaisha chaji kwa haraka zaidi pale unapocheza game hiyo kwenye simu yako.

Kuzima na kuwasha simu yako kusaidia kuondoa programu hizo kwenye simu yako na kusaidia simu yako kuanza upya, hii ni sawa na wewe unapo pumzika kila siku jioni baada ya kazi za kutwa nzima. Ndio maana nilisema pale mwanzo “kila kitu huchoka” hata simu yako pia inachoka.

Na hizo ndio sababu chache na muhimu ambazo zinaweza kukufanya kuona kuwa ni muhimu ku-restart simu yako angalau mara moja kwa wiki. Kama unataka kujifunza mambo mengine mengi ya teknolojia, unaweza kuanzia hapa kwa kujifunza mambo ambayo ni hatarishi kwa battery ya simu yako.

Kwa habari na mafunzo mbalimbali ya teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia usisahau ku-subscriber kwenye channel yetu kwani huwa tunajifunza maujanja mbalimbali kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use