Kampuni maarufu ya biashara ya kuuza bidhaa mtandaoni kwa barani Afrika Jumia, hivi karibuni imetangaza kusitisha huduma zake kwa hapa Tanzania. Kwa mujibu wa tovuti ya Techweez, Jumia Tanzania imetengaza kusitisha huduma zake rasmi kuanzia siku ya Jana tarehe 27 mwezi wa 11 mwaka huu 2019.
Kwa mujibu wa maelezo ya sababu ya kusitisha huduma zake hapa Tanzania, Jumia Tanzania imefikia uamuzi huo mgumu baada ya kuona mafanikio madogo kwa upande wa hapa Tanzania ukilinganisha na uwekezaji na uendeshaji wa huduma zake. Maelezo hayo yalikuwa yakitafsiri.
“Kwa kuzingatia mapitio yetu ya njia ya kufaulu, tumefanya uamuzi mgumu wa kukomesha shughuli zetu nchini Tanzania ifikapo tarehe 27 Novemba 2019.
Wakati Tanzania ina uwezo mkubwa na tuna jivunia ukuaji ambao tumeona pamoja kutokana na kukubaliwa kwa Jumia, lazima tuzingalie rasilimali zetu kwenye masoko yetu mengine. Uamuzi huu sio rahisi lakini utasaidia kuweka umakini wetu na rasilimali mahali ambapo tunaweza kusaidia Jumia kustawi zaidi.
Jumia itaendelea kusaidia wanunuzi na wachuuzi kupitia tovuti zetu za matangazo ya kuuza na kununua, ambayo hapo awali ilikuwa ikitwa Jumia Deals, ambayo sasa itakuwa ndio tovuti kuu pale unapo ingia kwenye tovuti ya jumia.co.tz. Maelfu ya wanunuzi na wachuuzi wanaofanya biashara kupitia portal hii na tunaamini itaendelea kuwa sawa katika siku zijazo“. Mwisho wa kunukuu.
Hata hivyo, hatua hii inakuja siku chache baada ya kampuni ya Jumia kutangaza kusitisha huduma zake kwenye nchi ya Cameroon ambapo pia inasemekana kuwa sababu ni kama hizi za kutoku pata faida inayo endana na uwekezaji.
Miezi kadhaa iliyopita, Kampuni ya Jumia ilitangaza kuingia kwenye soko la hisa la Marekani (NYSE), ambapo hisa zake zilipanda kwa haraka na baadae kushuka kwa kasi baada ya kuanza kuibuka kwa taarifa za udanganyifu ambazo zinasemekana kutolewa na kampuni hiyo kabla ya kujiunga na soko hilo kubwa la hisa duniani.
Kwa sasa tovuti ya jumia.co.tz imebadilishwa kabisa na utakapo ingia kwenye tovuti hiyo utapelekwa kweye tovuti ya Jumia Deals ambayo kwa sasa inaruhusu watumiaji kuuza na kununua kama tovuti ya kupatana. Huduma nyingine za Jumia kama Jumia Food, Jumia Travel zote bado zinaonekana kuendelea kufanya kazi kwa hapa Tanzania.
Ahsanteni kwa habari nzuri kila siku.
Shukrani kwa kuendelea kutujuza habari kila siku