Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wake wa Instagram, hivi karibuni imetangaza ujio wa app mpya ya Threads kwa ajili ya watumiaji wa Android na iOS. Threads imetengenezwa maalum kuruhusu watumiaji wa instagram kuchati, pamoja na kushiriki picha na video kwa urahisi zaidi baina ya vikundi vya watu walio karibu zaidi yaani (Close Friend).
Mwaka jana 2018, Instagram ilitangaza ujio wa magroup ya marafiki wa karibu kupitia instagram yaani close friend, magroup haya huruhusu mtumiaji wa instagram kuweza kushiriki picha au video na watu wake wa karibu waliopo kwenye list hiyo ya Close Friend. Sasa app hiyo mpya ya Threads ni kwa ajili ya listi hiyo ya marafiki.
Kupitia app hiyo mpya, mtumiaji ataweza kushare Status, picha na video kwa urahisi zaidi na kikundi chake cha marafiki ambao wapo kwenye list hiyo ya Close Friend, kama huna listi ya marafiki hao kwenye akaunti yako ya Instagram app hii itakuruhusu kutengeneza list hiyo kabla ya kuanza kutumia.
Jinsi ya Kutumia App ya Threads by Instagram
Kama bado huja pakua app hii mpya basi unaweza kufanya hivyo kwa kudownload kupitia soko la Play Store au App Store kwa kubofya link hapo chini.
Threads from Instagram – Android
Threads from Instagram – iOS
Baada ya kupakua app hiyo na ku-install vizuri kwenye simu yako, sasa endelea kwa kufungua app hiyo. Baada ya kufungua utaletwa moja kwa moja kwenye ukurasa ambao unakutaka kuchagua akaunti ambayo unataka kutumia nayo app hiyo mpya ya Threads.
Chagua akaunti hiyo kwa kubofya Continue as au bofya sehemu ya Switch Accounts kama unataka kubadilisha akaunti kama unayo akunti zaidi ya moja kwenye app yako ya Instagram.
Baada ya kuingia kwa kutumia akaunti yako, kama bado huna listi ya marafiki wa karibu yaani Close Friend kwenye akaunti yako ya Instagram app hii itakupa nafasi ya kuchagua marafiki kwa kuweka alama ya tiki mbele ya jina la akaunti ya mtu kisha utaweza kutengeneza listi ya Close Friends. Kama tayari unayo listi hii basi utapelekwa kwenye hatua inayofuata.
Hatua inayofuata unatakiwa kuwasha sehemu ya Auto Status, sehemu hii inaruhusu app hiyo kuweka Status ya maneno pembeni ya profile yako na hii hufanywa kulingana na eneo unalo kwenda. Ili kutumia sehemu hii ya Auto Status unatakiwa kuwasha Location kwenye simu yako, pia unaweza kuchagua Status mwenyewe kila mara unapo tumia app hiyo.
Baada ya hapo sasa utakuwa uko tayari kuanza kutumia app hii mpya ya Threads from Instagram, app hii ni kama vile Snapchat na ina angalia zaidi sehemu ya Stories hivyo unaweza kutumia app hii kama ilivyo sehemu ya Stories lakini hii itakuwa bora zaidi kwani utapewa uwezo wa kuchat na kushiriki video na picha na marafiki zako wa karibu.
Kama una mahali ambapo utakwama usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini, nasi tutakuelekeza moja kwa moja jinsi ya kutumia app hii mpya. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.
nice