Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania

Utaweza kubadili Camon Series kwa Camon 12 na kiasi cha TZS 203,463
TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania

Wateja wa TECNO sasa kunufaika na ujio wa toleo jipya la TECNO Camon 12, Camon 12 Air na Camon 12 Pro pamoja na kauli mbiu mpya ya TECNO EXPECT MORE.

Kauli mbiu ya TECNO EXPECT MORE inathibitisha juu ya ujio wa matoleo mapya kuwa na ubora zaidi kama ilivyo kwa toleo jipya la TECNO Camon 12 lakin vile vile ujio wa TECNO Camon 12 unaashiria mapinduzi katika mfumo wa kidigital kupita kamera yake yenye 16MP AI Max Rear Triple Camera.

Advertisement

TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania

Akizungumza wakati wa uzinduzi, afisa wa mahusiano wa TECNO Mobile Tanzania Bwana Eric Mkomoye alisema kwamba, “mageuzi ya kiteknolojia kutoka analojia kwenda digitali yawezekana kama sifa zote zinazotumika zinapatikana kiganjani mwako kama vile kamera nzuri, battery yenye nguvu, uwezo mkubwa wa kuhifadhi data na muonekano mzuri wa kipekee”, Bwana Mkomoye, aliorodhesha sifa za TECNO Camon 12 kama zifuatazo; “16MP+2MP+8MP Rear camera with quad flash, 16MP AI Clear Selfie, GB 64+GB 4,4000mAh battery, 6.52″ Crystal Dot Notch Screen, 4G na Android 9 Pie”.

TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania

Vile vile aligusia kuhusiana na kauli mbiu mpya ya TECNO EXPECT MORE na ofa inayopatikana katika camon 12 kwa kusema ni muda mrefu sasa wadau wa TECNO wameshuhudia mengi ikiwamo simu zetu zenye kubeba sifa za hali ya juu katika bei Rafiki na sasa tumeona ni muda waku tegemea mapinduzi yenye ubora zaidi ya awali na kuhusiana na ofa TECNO imewapa nafasi watumiaji wote wa TECNO camon series kubadili kwa TECNO camon 12 kwa kiasi cha shilling 203,463 za kitanzania. Unaweza kusoma zaidi hapa kujua zaidi kuhusu vigezo na masharti.

TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania
Wakati wa uzinduzi mmoja wa mawakala wa TECNO, Bw.Abuyi alituelezea uzoefu wake wakufanya kazi na TECNO kuanzia ilipoanzaishwa nchini Tanzania, alieleza zaidi kuhusu furaha yake kuiona TECNO kupiga hatua kubwa pia imesaidia wafanyabiashara kufanikiwa katika soko.

Uzinduzi huu uliudhuriwa na wadau kutoka sekta mbalimbali mfano, masoko,mauzo na teknolojia. Kutoka upande wa masoko na mauzo alikuepo mkurugenzi mtendaji wa Airtel Bw.George Mathen pamoja na Afisa Masoko wa Airtel Bw. Amit Chandiramani, Mkurugenzi mtawala wa TIGO Bw.Simon akiwa na Afisa Masoko Bw.Tariq na kutoka Vodacom alikuwepo Mkurugenzi mtawala Bw.Hashim Hendi na Mragahabishi ambaye pia ni mpiga picha Bw.Osse Greca Sinare.

TECNO Yazindua Simu Mpya za Camon 12 Nchini Tanzania

Tofauti na Uzinduzi ,shughuli nyingine kama burudani kutoka kwa wasanii na droo ya kubahatisha vilifanyika ambapo wageni waalikwa walipata nafasi kujishinda toleo jipya la simu aina ya TECNO Camon 12 papo kwa hapo.

TECNO inajivunia kutengeneza na kusambaza simu janja zenye ubora na matumizi Rafiki kwa mazingira husika. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya TECNO Mobile Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use