Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Simu hii inakuja na kamera nne na mtindo mpya wa kioo chenye kitobo
Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5 Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Hatimaye hivi leo oktoba 15, 2019 kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix S5 huko nchini India. Infinix S5 ni mrithi wa simu ya Infinix S4 ambayo ilizinduliwa hapa Tanzania takribani miezi mitano iliyopita.

Infinix S5 inakuja na muundo mpya kabisa wa kioo huku ikiwa na sehemu ya kamera ya mbele iliyopo ndani ya kioo au (Punch hole display), kioo hicho kime tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku kikiwa na urefu wa jumla ya inch 6.6 pamoja na resolution ya hadi pixel 720 x 1520.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Advertisement

Simu hii inakuja na kamera za nne za nyuma, kamera kuu inakuja na 16-megapixel, nyingine zina kuja na megapixel 5 ambayo ni ultrawide, megapixel 2 ambayo ni depth sensor na megapixel 2 nyingine ambayo ni low-light. Kamera zote zina kuchukua video hadi 1080p@30fps. Kwa upande wa sifa za kamera ya mbele Infinix S5 haina tofauti na Infinix S4 kwani nayo inakuja na kamera ya selfie ya yenye megapixel 32.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Simu inakuja na chipset ya MediaTek MT6761 Helio P22 na nguvu ya CPU ya Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A53 na 4×1.5 GHz Cortex-A53). CPU hiyo inasaidiwa na RAM ya hadi GB 4 na uhifadhi wa ndani wa hadi 64 GB. Hifadhi ya hiyo ya ndani inaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Infinix S5 ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix S5

Soma hapa Sifa kamili za simu hii

Bei ya Infinix S5

Kwa upande wa bei Infinix S5 inatarajiwa kuingia sokoni nchini India hivi karibuni na inasemekana kuuzwa kwa rupee ya india ₹10,999 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania TZS 354,000 bila kodi. Simu hii ina tegemewa kuuzwa kwenye soko la flipkart kwa bei ya punguzo.

12 comments
  1. Kiukweli sim nzuri Sana infinix naitumia haijawahi kuharbija wara kusumbuaa hata kdogo Ila naitaji iyo S5 naipataje nipo dodoma

  2. Je in 4G lite make infinix sim zao haziwekei 4Gkama inayo 4G nicheckini no:0628811117/ whatsap 0629174478 naitaji infinix

  3. Kwanini infinix s5 ukipigiwa na ukipokea au kupiga ukiisogeza sikio sensor haifanyi kazi kioo kuzima au kuna setting, nini tatizo wataalamu au ndo muundo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use