YouTube ni moja ya mitandao yenye faida kubwa sana hasa kwa watu wanaopenda kujifunza mambo mbalimbali, binafsi nimeshaona watu wengi sana wakianzisha biashara pamoja na makampuni makubwa mara baada ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia mtandao wa YouTube.
Sasa kuliona hilo leo nimekuletea makala ambayo inaweza kukusaidia sana kufanikiwa hasa kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kujifunza programing.
Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha channel bora za YouTube ambazo zinaweza kusaidia wewe kujifunza jinsi ya kutengeneza website, programu (apps) pamoja na mambo mengine mbalimbali yanayohusu programing.
Channel hizi zinaweza kusaidia sana kwani kwa upande wangu zimenisaidia sana na bado zina endelea kunisaidia, kupitia makala hii nita kueleza njia bora za kutumia channel hizo ili kuweza kujifunza kwa urahisi, basi bila kupoteza muda zaidi basi twende tuka angalie channel hizo.
TABLE OF CONTENTS
FreeCodeCamp.org
FreeCodeCamp.org ni moja kati ya channel bora sana za kujifunza kutengeneza programu mbalimbali pamoja na website. Channel hii huonyesha video nzima za jinsi ya kutengeneza programu kwa kutumia lugha mbalimbali za kompyuta, unaweza kujifunza kutengeneza programu kupitia video moja kwa kuangalia mwanzo hadi mwisho kitu cha muhimu tu hakikisha unao muda wa kutosha kwani video moja inaweza kuwa na masaa hata zaidi ya matatu.
Derek Banas
Derek Banas ni channel nyingine ambayo ni bora sana hasa kwenye ulimwengu wa programing, kupitia channel hii pia unaweza kujifunza jinsi ya kutumia lugha mbalimbali za kompyuta kutengeneza programu mbalimbali kwa haraka, utofauti wa channel hii ni kuwa kuna wakati inapakia video za mafunzo ya mambo ya masoko na vitu vingine kama hivyo.
Hitesh Choudhary
Hitesh Choudhary ni channel nyingine bora ya kujifunza jinsi ya kutengeneza apps pamoja na website, channel hii ni tofauti kidogo kwa sababu kupitia hapa utajifunza mambo mengi mbalimbali kama vile nini maana ya API, API inafanyaje kazi.? pamoja na mambo mengine mbalimbali. Channel hii ni nzuri sana kwa wale ambao wanataka kujifunza programing kwa ujumla na sio tu upande wa apps pamoja na website.
ProgrammingKnowledge
Programming Knowledge ni channel nyingine bora kwa ajili ya kujifunza kutengeneza programu na website, channel hii ni bora kwa sababu inafundisha zaidi kutengeneza website kwa kutumia lugha za PHP na lugha nyingine za kompyuta, kama unataka kujifunza kutengeneza programu mbalimbali za mtandaoni basi channel hii ni bora sana kuitembelea.
Coding in Flow
Channel nyingine ambayo ni bora kwa kujifunza kutengeneza programu ni pamoja na Coding Flow, channel hii ni bora sana kama unataka kujifunza kutengeneza apps za Android. Channel hii ina video zenye makala zinazo fundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza programu kwa urahisi, kizuri kuhusu channel hii ni kuwa unaweza kujifunza hata kama ndio mara yako ya kwanza una anza kujifunza programing.
Programming with Mosh
Programming with Mosh ni channel nyingine ambayo itakusaidia sana kujifunza programing, kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kujifunza lugha mbalimbali za kompyuta kama vile python, javascript, C++ na csharp basi channel hii ni bora sana kwako. Uzuri wa channel hii ni kuwa ina angalia zaidi kwa watu ambao ndio wana anza kujifunza hivyo kama hii ndio mara yako ya kwanza kwenye ulimwengu wa programi basi channel hii ni bora kwako.
Academind
Channel nyingine bora kwa kujifunza programing ni pamoja na Academind, hii ni channel ambayo nayo pia itakuapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu programig ikiwa pamoja na jinsi ya kutengeneza app pamoja na website kwa kutumia lugha mbalimbali kama vile React Native, Ionic pamoja na Android Studio. Kama unataka kujifunza kutengeneza programu huku ukipata elimu mbalimbali basi ni vyema kutembelea channel hii.
edureka!
Edureka ni channel nyingine nzuri sana kwa ajili ya kujifunza programing ikiwa pamoja na jinsi ya kutengeneza programu mbalimbali. Channel hii ni nzuri sana kwa sababu inakupa video ambazo ziko kwenye mfumo wa kozi mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kujifunze kutengeneza programu pamoja na website.
Na hizo ndio baadhi ya channel ambazo kwa upande wangu nazifuatilia sana na ambazo nadhani zinaweza kukusaidia kujifunza kitu kama unataka kuwa mtaalamu wa kutengeneza apps pamoja na website.
Kumbuka elimu haina mwisho hivyo hata kama wewe ni mtaalamu kiasi gani ni vyema kujua kuwa wapo wataalam zaidi yako hivyo ni muhimu kuendelea kujifunza zaidi na zaidi hasa kwa watu ambao unadhani hawajui kama wewe.
Mpaka siku nyingine guys.. kama unajua channel nyingine bora kwaajili ya kujifunza programing basi unaweza kuzitaja kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujua tovuti nyingine bora ambazo zinafanana na Youtube ambazo unaweza kuzitumia kupata pesa mtandaoni basi soma makala hii hapa.