in

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako

Utaweza kubaki na namba yako hiyo hiyo lakini mtandao utabadilika

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako

Kadri siku zinavyokwenda teknolojia inazidi kusonga mbela na mambo mengi ambayo zamani yalikuwa hayawezekana kwa sasa yana wezekana kwa urahisi kabisa. Kwa hapa Tanzania ilikuwa ni lazima mtu kubadilisha laini ya simu pale anapotaka kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwendalakini kwa sasa sio lazima kufanya hivyo kwani unaweza kuhamia mtandao mwingine bila hata kubadilisha line yako ya simu.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (MNP) au Mobile Number Portability ni “huduma ambayo itakuwezesha kubadili mtoa huduma wako wa simu za kiganjani Tanzania na kubakia na namba yako ileile”.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako

Huduma hii inakuwezesha kubakia na namba yako bila kujali unatumia mtandao gani hivyo kukuondolea adha ya kutoa taarifa kwa watu wako wa karibu pale unapobadili mtoa huduma wa simu za kiganjani. Kwa kuwa namba yako ya simu itabaki ilele, basi itakuwa ni kitambulisho chako, yaani NAMBA YAKO, UTAMBULISHO WAKO.

Faida za (MNP) Mobile Number Portability

Kwa mujibu wa TCRA, huduma hii ambayo imezinduliwa tokea mwaka 2017, itakusaidia kuweza kubadilisha watoa huduma pamoja na faida nyingine kama –

  • Kubaki na namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine.
  • Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona anatoa huduma bora zaidi, huduma nzuri kwa wateja, anakidhi matarajio yako na ana ubunifu katika kutoa huduma zake.
  • Kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno bila kujali ni mtandao upi umehamia bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako.
  • Kuokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja.

Mbali na faida nyingi zinazopatikana kwa kutumia huduma hii hapa nchini Tanzania, vipo vigezo na masharti ambayo unahitaji kuvifuata ili kuhakikisha unaweza kupata na kutumia huduma hii ya kubadilisha mtandao wa simu bila kubadilisha namba yako ya simu.

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako

Masharti ya Kupata Huduma ya Mobile Number Portability

Mfumo wa kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani utatumiwa na wateja wote nchini wanaolipia huduma kwanza na wanaolipia huduma baada ya matumizi. Ili kuingia kwenye mfumo huu, simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika, yaani haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.

Iwapo ni mtumiaji anayelipia kabla ya huduma, yaani Prepaid :-

  • Hutaweza kuhama na namba ambayo imefungiwa au kusimamishiwa huduma;
  • Hutaweza kuhama na salio lililopo na utatakiwa kutumia salio hilo kabla ya kuhama la sivyo salio lako litapotea;
  • Hutaweza kuhama iwapo una mkopo kutoka kwa mtoa huduma wako hapa nchini kama vile chini ya mfumo wa M-pawa na NipigeTafu au mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi, pesa mtandao na kadhalika;
  • Hutaweza kuhama iwapo namba yako inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.
  • Hutaweza kuhama iwapo una mkopo kutoka kwa mtoa huduma wako hapa nchini kama vile chini ya mfumo wa M-pawa na NipigeTafu au mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi, pesa mtandao na kadhalika
  • Hutaweza kuhama iwapo namba yako inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.

Kwa taarifa zaidi za vigezo na masharti zaidi ya huduma hii ya Mobile Number Portability, hakikisha UNAPAKUA HAPA nyaraka yenye vigezo na masharti yote kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mbali na hayo ni vyema kuzingatia kuwa, Hakuna gharama za kuhama na namba yako isipokuwa. Hata hivyo, kabla ya kuhama itabidi ununue laini mpya ya simu ya kiganjani, yaani “SIM card” kutoka kwa mtoa huduma mpya.

Wateja wote wanaotaka kuhama na namba zao na ambao wana salio katika akaunti ya pesa mtandao ni lazima walitoe salio hilo kabla ya kuhama vinginevyo salio litabaki bila mwenyewe na itabidi wafuate mchakato mrefu ili kuweza kupata pesa zao ambazo wakati wote zitakuwa salama hadi watakapokamilisha mchakato huo.

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako

Jinsi ya Kuhama Mtandao Bila Kubadilisha Namba

  • Nenda vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma unakotaka kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungependa kuhama na namba yako.
  • Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi (fomu moja).
  • Sehemu ya Fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa utawajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali kama yapo.

Utatakiwa kutoa vitu vifuatavyo: –

  • Kitambulisho chenye picha yako – kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.
  • Simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba unayotaka kubaki nayo.
  • Iwapo una salio katika akaunti ya pesa mtandao utashauriwa kutoa pesa kabla ya kuhama ili kuepuka usumbufu kama ilivyoelezwa kwenye masharti ya kuhama.
  • Utatakiwa kutuma meseji yenye neno “HAMA” kwenda namba ‘15080’ ambayo ni namba maalum ya kuhama. Msaada utatolewa iwapo utahitajika ili kufanikisha hili.
  • Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa.
  • Iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na kutokukamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali, maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya mchakato huu.
  • Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu za kiganjaji atakupatia laini mpya.
  • Ili kuzuia kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama, huduma za kifedha zitasitishwa kwa muda mpaka namba ikapohamishwa kwa mtoa huduma mpya, ambapo utatumia huduma zake za fedha mtandao kama utajiunga na huduma zipo.
  • Katika kipindi cha kuhama huduma za kupiga na kupokea simu na ujumbe mfupi zitaendelea kama kawaida.
  • Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka, mara nyingi siku hiyo hiyo au, iwapo utachelewa sana, ndani ya siku mbili za kazi baada ya kukamilisha utaratibu wa maombi. Wakati huo namba yako itakuwa imeshahamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini yako ya awali haitatumika tena. Utatumiwa ujumbe mfupi kuwa uhamaji umekamika na ubadilishe laini.
  • Ikifikia hapo, weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu yako. Iwapo huna uhakika wa nini cha kufanya, unaweza kwenda kwa mtoa huduma wako mpya au wakala wake au kuwapigia simu na wataweza kukusaidia.
  • Mchakato umekamilika.

Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kubadilisha mtandao wa simu bila kubadilisha namba yako ya simu, kwa habari zaidi hakikisha unapitia tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwaajili ya kupata taarifa zaidi.

Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu Bila Kubadilisha Namba Yako
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.