Kampuni ya Samsung hivi leo imezindua simu mpya ya Galaxy M30s, simu ambayo ni toleo la maboresho ya simu ya Galaxy M30 ambayo ilitoka mapema mwaka huu 2019. Simu hii mpya ya Galaxy M30s inakuja na maboresho mengi sana ikiwa pamoja na battery, uwezo wa kamera pamoja na uwezo wake kwenye processor pamoja na mambo mengine.
Kwa sababu hili ni toleo la maboresho sitopoteza muda mwingi kuandika kuhusu sifa za awali za simu hizi na badala yake moja kwa moja tutaenda kuangalia sifa pamoja na bei ya simu hii mpya
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Samsung Galaxy M30s
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400 pixels, pamoja na uwiano wa 19:9 ratio (~411 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9611 (10nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP3.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.9, 1/3.1″, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 1/5″, 1.12µm, depth sensor na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 5. Kamera zote zinauwzo wa kuchukua video za 4K
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 6000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Opal Black, Sapphire Blue, Pearl White.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Samsung Galaxy M30s
Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy M30s inategemewa kuanza kupatikana kwa nchini India kwa rupee ya india Rs.13,999 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania TZS 453,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 4 na ROM ya GB 64. Toleo lenye RAM ya GB 6 na ROM ya GB 128 litauzwa kwa rupee ya India Rs.16,999 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania TZS 549,000 bila kodi. Kumbuka bei za simu hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania kutoka na kodi pamoja na viwango vya kubalisha fedha.