Jinsi ya Kupewa Haraka Matangazo ya Adsense Kwenye Blogger

Hizi hapa njia 5 za muhimu ambazo unaweza kuzifuata
Jinsi ya Kupewa Haraka Matangazo ya Adsense Kwenye Blogger Jinsi ya Kupewa Haraka Matangazo ya Adsense Kwenye Blogger

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki tovuti ya blogger najua kabisa umewahi kujaribu kuomba matangazo ya Adsense kwenye blog yako bila mafanikio. Sasa kupitia makala hii naenda kuonyesha mambo ya msingi ambayo ukiyafanya utaweza kupewa matangazo ya Adsense kwenye blog yako kwa haraka.

Kumbuka njia hizi ni muhimu sana kama unatumia mtandao wa blogger kwa lugha ya kiingereza kwani itakuwa ni rahisi zaidi kuweza kukubaliwa maombi yako kwa haraka zaidi. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie mambo haya.

Advertisement

1. Nunua Domain (Custom Domain)

Ni ukweli usio pingika kuwa mara nyingi vitu vya bure huruhusu watu kutokuwa na bidii na hivyo watumiaji hutumia vitu hivyo ovyo kwa sababu tu hawaja ingia gharama. Kwa upande wa blogger nayo pia ni desturi kuona watu wengi wakianzisha blog lakini ni watu wachache sana huweza kufikisha miezi kadhaa na kuendelea kupost kwenye blog zao bila kuchoka.

Mara nyingi pale unapo nunua domain na kuunganisha na blogger yako, Google huchukulia hii kama hatua ya muhimu kwa biashara ya uhakika kwani usingeweza kununua domain kama huna uhakika na biashara hiyo au blog yako. Mara nyingi ni ngumu domain ya blogspot kupewa matangazo na hata ikipewa matangazo inaweza kukaa miezi kadhaa na ukaona matangazo yamezimwa. Unaweza kununua domain kwa Tsh 3000 hapa

2. Post Makala Zaidi ya 10 au 15 Kwanza

Kitu kingine cha msingi ni kuhakikisha una post makala zaidi ya 10 ambazo zimeandikwa kwa ubora wa hali ya juu na pia hakikisha makala hizi zina maneno mengi angalau zaidi ya maneno 400 kwa post moja. Pia ni vizuri kuandika makala zenye akili na zenye kutoa msaada kwa watu kwani Google inajua jinsi ya kuangalia makala hizo na kujua kama umeandika tu ilimradi upewe matangazo. Kama unapatashinda kuandika makala ndefu hakikisha unaweka picha na video zilizopo ndani ya mada unayo andikia hata kama sio video zako mweyewe.

Pia ni vyema kuhakikisha uchukui makala ya mtu yoyote kwani Google pia wanajua jinsi ya kuangalia kama makala uliyo andika kama imechukuliwa kutoka kwenye tovuti nyingine. Pia hakikisha picha unazotumia huzitoi kwenye tovuti nyingine yani copy + paste bali jitahidi kuedit picha hata kama umeichukua kwenye mtandao mwingine. Pia unaweza kupata picha za bure za kutumia kupitia tovuti kama pixabay.com , pexels.com

3. Kurasa za Mawasiliano, Kuhusu, Sera ya Faragha na Vigezo na Masharti

Hakikisha kwenye tovuti yako kuna kurasa za muhimu kama kurasa za mawasiliano (Contact us), Kuhusu sisi (About Us), Sera ya Faragha (Privacy Policy) pamoja na Vigezo na Masharti au (Terms and Conditions). Kurasa hizi pia zinaeleza kama uko na uhakika na biashara yako ndio maana umeweka kurasa hizo kwani umeona uhitaji wake.

Hakikisha unaweka kurasa hizi kabla ya kuomba matangazo kupitia blogger kwani hii itakusaidia sana kuruhusiwa haraka kuanza kuonyesha matangazo. Kama huwezi kutengeneza kurasa za namna hii unaweza kutumia tovuti maarufu kama termsandconditionsgenerator.com.

4. Hakikisha Blog yako Inakuwa na Muundo Bora

Kwa hapa Tanzania sio jambo la kushangaza kuona blog zinazotumia blogger kufanana hasa kwa muundo, hii husababisha blog kuonekana kama zinafanana na kufanya Google kushindwa kuruhusu matangazo kwenye tovuti hizo kwa haraka. Hakikisha unatumia templent ambayo ni bora na yenye muonekano mzuri bila kusahau yenye kufanya kazi kwa haraka zaidi. Kama unataka templents nzuri kwaajili ya blog yako unaweza kupata templent kwenye tovuti kama gooyaabitemplates.com

5. Subiri kwa Muda Kabla ya Kuomba Matangazo

Mara nyingi watu wengi hufanya kazi za kutengeneza blog kwaajili ya kupata pesa hivyo huwa hawana subira hata kama blog hiyo ni mpya. Kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuhakiksha unaendelea kupost kwenye blog yako kabla ya kuomba matangazo ya Adsense angalau subiri kwa mwezi mmoja ndio uweze kuomba matangazo kwa mara ya kwanza. Ndani ya mwezi huo hakikisha blog yako inapatikana kwenye Google search na hasa pale unapo tafuta jina la blog yako bila kuweka blogspot.com.

Kama unataka kupewa matangazo kwa haraka zaidi hakikisha una ongeza makala nyingi hata zaidi ya 25 kisha subiri kwa muda wa miezi miwili kisha omba matangazo kwa kutumia akaunti yako ya Adsense. Kumbuka ni vyema kuomba matangazo kwa kutumia akaunti ya adsense ambayo ipo kwa muda mrefu kwani Google huchukua muda kuruhusu akaunti ya matangazo.

Na hayo ndio mambo ya muhimu ambayo ukiyafuata na kuhakikishia utapewa matangazo na Google ndani ya masaa kadhaa. Kumbuka unahitaji traffic ya kutosha angalau watu 100 kwa siku kwenye blog yako ili kupata matangazo hivyo fanya kazi ya ku-post zaidi ndio baadae uangaike na matangazo. Najua kuna baadhi ya watu hawajapenda hii kwa kuwa ni kazi ngumu ila ukweli ndio huo, kwa elimu zaidi hakikisha unasoma makala itakayo kujuza kuhusu faida za matangazo ya Google Adsense kwa Tanzania.

Mpaka siku nyingine hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, nami nakutakia mafanikio mema kwenye safari yako ya kutengeneza pesa kwa kutumia Google Adsense…

7 comments
  1. Sasa ww unafundisha kuhusu kupata Adsense approved akati hauna Ata matangazo ya kutengeza mwenyewe tunakuamini vp embu wape watu unachoona unauwezo nacho sio unakurupuka

    1. Tumeshafanya kazi kwenye blog za makampuni mbalimbali ikiwa pamoja na watu wengi binafsi, hayo ndio baadhi ya mambo ambayo tulifanya kwenye blog hizo na kupewa matangazo bila kusumbuliwa.

  2. Nahitaji kuunganishiwa matangazo ya kulipwa kwenye blog yangu ya MACHWEO COMMUNICATION NEWS

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use