Hivi karibuni WhatsApp ilileta sehemu mpya ya ulinzi kwa alama za vidole kwenye programu yake ya mfumo wa iOS. Sasa hivi karibuni tegemea kupata sehemu hiyo kupitia simu za mfumo wa Android.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, sehemu hiyo itasaidia kuongeza ulinzi kwenye programu hiyo kwani kila mara ambapo utakuwa unataka kuingia kwenye programu hiyo, utaletewa ujumbe wenye kutaka kuweka alama ya kidole kupia sehemu hiyo ya fingerprint kwenye simu yako.
Pale mtumiaji anapowasha sehemu hiyo, mtu yoyote hatoweza kuona meseji zinazo ingia hata kama zikija kwa njia ya Notification au kupitia widget maalum inayowekwa juu ya kioo. Kama ikitokea mtu anataka kusoma meseji bila kuweka alama ya kidole basi ataletwa ujumbe ulio andikwa “content is hidden due to fingerprint lock”.
Vilevile kutakuwa na sehemu mpya ya mpangilio (Settings) ambayo itakuruhusu kuchagua ni wakati gani unapotaka sehemu hiyo iweze kujiwasha mara baada ya kumaliza kutumia programu hiyo. Unaweza kuchagua programu hiyo ijifunge yenyewe haraka unapo maliza kuchati na kufunga programu hiyo, au unaweza kuchagua ijifunge baada ya dakika moja au baada ya nusu saa.
Sehemu hii kwa sass ipo kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta, na pengine tegemea kuona sehemu hiyo kwenye programu ya Android siku sio nyingi. Kama unayo programu ya majaribio ya WhatsApp unaweza kupata sehemu hiyo kupitia sehemu ya Settings kisha bofya sehemu ya Privacy alafu utaona sehemu ya Fingerprint lock bofya hapo kuweza kuwasha sehemu hiyo.
Kupata taarifa zaidi kuhusu ujio wa sehemu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unapakua app yetu ya Tanzania Tech kama bado hujafanya hivyo.
Tayari hiyo huduma ya Fingerprint kwenye WhatsApp inafanya kazi
Unatumia simu ya mfumo gani..? Android au iOS.?
Phantom 9 bei gani
Kuanzia 750,000 hadi 780,000