Habari mpya wiki hii zinadai kuwa, huwenda kampuni ya Infinix ikazindua simu mpya ya Infinix Hot 8 mwezi ujao. Infinix Hot 8 itakuwa ni toleo la maboresho ya simu ya Infinix Hot 7, simu ambayo ilizinduliwa mapema mwezi January mwaka huu 2019.
Kwa mujibu wa tetesi kutoka tovuti ya 91mobile, simu hiyo mpya inasemekana kuja na muonekano unao fanana na Infinix Hot 7 ikiwa pamoja na kioo ambacho kinasemekana kuja na muundo sawa Hot 7 huku ikiwa na ukingo wa juu maarufu kama water drop notch.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo ambayo walifanikiwa kupata picha ya box la simu hiyo, Infinix Hot 8 inasemekana kuja na ukubwa wa ndani au ROM GB 64 pamoja na RAM ya GB 4 pamoja na uwezo wa mtandao wa 4G LTE. Vile vile kama unavyoweza kuona simu hiyo inakuja na kioo chenye ukingo wa juu maarufu kama water drop notch.
Kwa upande wa sifa nyingine bado haija julikana ila inadaiwa kuwa simu hii inaweza kuja na processor bora kuliko Infinix Hot 7. Vilevile inasemekana kuwa simu hii itazinduliwa mara ya kwanza nchini India na itakuwa inauzwa chini ya rupee ya india Rs 10,000 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 321,000 bila kodi, kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.
Kupata habari zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakupa habari pale simu hiyo itakapo kuja hapa nchini Tanzania.