Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kama tayari unajua sifa za Note 10, hizi hapa sifa za Note 10+
Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+ Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Baada ya kuangalia sifa za Galaxy Note 10, hebu sasa twende tukangalie sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy Note 10+. Kifupi ni kuwa, Galaxy Note 10 na Note 10+ zote zimezinduliwa siku ya jana tarehe 7 ya mwezi wa nane mwaka huu 2019 na zinategemewa kuingia sokoni siku chache baada ya kuzinduliwa hapo siku ya jana.

Samsung Galaxy Note 10+

Advertisement

Galaxy Note 10+ ni simu ambayo pengine ndio simu bora ya Samsung hadi sasa “kwa mtazamo wangu”, simu hii inakuja na kila sifa ambazo pengine mtumiaji mahiri wa smartphone unahitaji. Kama wewe ni mpenzi wa kamera basi Note 10 inayo kamera bomba, kama wewe ni mpenzi wa kioo kikubwa basi pia Note 10+ inakuja na kioo kikubwa ikiwa pamoja na battery kubwa na mambo mengine mengi ya zaidi, kwa kuwa makala ni ndefu kidogo hebu nisikuchoshe na twende tukangalie yote yaliyomo kwenye simu hii.

Kioo

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Galaxy Note 10+ inakuja na kioo cha inch 6.8 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED huku kikiwa na resolution ya hadi pixels 1440 x 3040. Kioo hicho kinakuja na teknolojia za ziada kama vile HDR10+, Always on pamoja na glass ngumu ya Corning Gorilla Glass huku ikiwa na sehemu ya fingerprint chini ya kioo.

Kamera ya Mbele

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kwa upande wa kamera ya mbele au selfie kamera, Note 10+ inakuja na kamera moja ya Megapixel 10, ambayo inakuja na uwezo wa kurekodi video za hadi pixels za 4K au maana nyingine ni sawa na kusema simu hii inauwezo wa kurekodi video za 2160p@30fps kwa kutumia kamera ya Selfie. Kama ilivyo Note 10 Kamera hiyo pia inakuja ikiwa inasaidiwa na teknolojia za Dual video call pamoja na Auto-HDR.

Kamera za Nyuma

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kama nilivyo kwambia, Kama wewe ni mpenzi wa kamera basi Note 10+ inakuja na kamera nne kwa nyuma, ambapo kamera kuu inakuja na Megapixel 12 ambayo hii ni wide lens, huku nyingine tatu zikiwa zinakuja na Megapixel 12 ambayo ni telephoto lens, nyingine Megapixel 16 ambayo ni ultrawide lens pamoja na kamera ya nne ambayo ni TOF 3D VGA kamera. Kamera zote hizi kwa ujumla zinaweza kuchukua video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za 2160p@60fps, 1080p@240fps pamoja na 720p@960fps.

Kamera za simu hii zinasaidiwa na Flash ya LED flash ambayo ipo sambamba na teknolojia za auto-HDR pamoja na panorama ambazo zipo kwenye kamera za nyuma za simu hizo.

Muundo

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kwa upande wa muundo Galaxy Note 10+ haina tofauti sana na Note 10, kwani 10+ inakuja na muundo unaofanana isipokuwa simu hii ni kubwa zaidi ya Note 10 na pia kwa nyuma inakuja na kamera nne na sio tatu kama ilivyo Note 10. Mengine yote yanafanana na Note 10 hivyo unaweza kusoma makala iliyo tangulia ili kujua zaidi kuhusu muundo huu.

Kalamu ya Galaxy Note 10+

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kalamu ya Note 10+ haina tofauti hata kidogo na Note 10, hivyo sitapoteza muda mwingi kukwambia maneno mengi kuhusu hili. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma makala iliyopita hapa. Na uhakika utaweza kujua ya msingi kuhusu kalamu hiyo.

Sifa za Galaxy Note 10+

Kwa upande wa Sifa Galaxy Note 10+ inakuja ikiwa na processor ya Exynos 9825 (7 nm) – EMEA/LATAM huku matoleo ya simu hii ambayo yatapatikana kwa nchi za china na Marekani yakiwa na processor za Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) – USA/China. Processor hizi zinasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 8 au GB 12, simu hii inakuja na ukubwa wa ndani au ROM ya kuchagua kati ya GB 256 au GB 512, unaweza kuongeza ukubwa huu kwa kutumia memory card ya Micro SD Card ya hadi Terabyte 1 (1 TB).

Galaxy Note 10+ pia inakuja na GPU ya Mali-G76 MP12 – EMEA/LATAM, huku matoleo ya China na marekani yakiwa yanakuja na GPU tofauti ya Adreno 640 – USA/China.

Mfumo wa Uendeshaji

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji Galaxy Note 10+ inakuja na mfumo wa Android 9 Pie, huku ikiwa na mfumo wa Samsung wa One UI ambao umeboreshwa zaidi. Vilevile Samsung inakuja na mfumo wa Samsung DeX, mfumo ambao unakuruhusu kutumia Simu hii kwenye kioo cha kompyuta kwa kuchomeka simu hiyo kwa kutumia waya maalum.

Uwezo wa Battery

Kwa upande wa battery Note 10+ inakuja na kubwa ya battery ya Li-Ion 4300 mAh, battery ambayo inakuja na teknolojia ya Fast battery charging ya hadi 45W. Mbali na hayo Note 10+ pia inakuja na teknolojia ya Fast Qi/PMA wireless charging ya hadi 20W.

Viunganishi na Mengine

Zijue Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10+

Kama ilivyo Note 10, Galaxy Note 10+ inakuja na radio kwa simu zitakazo patikana nchin marekani na China, lakini kwa simu zitakazo patikana hapa Afrika inawezekana kabisa zisiwe na Radio. Simu hii pia inakuja ikiwa haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, na sasa inakubidi kutumia headphone za Type C ambazo zinachomekwa sehemu moja na sehemu ya chaji ambayo inatumia USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.

Simu hii pia inakuja na Wifi ya Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac/ax, dual-band yenye uwezo wa Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth ya 5.0, A2DP, LE, aptX pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya NFC. Mbali na hayo Note 10+ inakuja na Sensor za Fingerprint (chini ya kioo), accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer na SpO2. Kwa upande wa rangi inakuja na rangi tatu za kuchagua za Aura Glow, Aura White pamoja na Aura Black.

Bei ya Galaxy Note 10+

Kwa mujibu wa Samsung, bei ya Galaxy Note 10+ ya GB 256 inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $1,100 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,530,000 bila kodi, Note 10+ ya GB 512 inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $1,200 ambayo ni sawa na Tsh 2,760,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania na Afrika nzima bei ya simu hizi inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Na hizo ndio sifa na bei ya Galaxy Note 10+, kama unataka kujua sifa kamili za Galaxy Note 10 basi unaweza kusoma makala iliyopita hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use