Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Hizi hapa sifa pamoja na bei ya Xiaomi Redmi Note 8 pamoja na Redmi Note 8 Pro
Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64 Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Kampuni ya Xiaomi hivi leo imeweka rekodi kupitia simu yake mpya ya Redmi Note 8 Pro, simu ambayo inabeba tuzo ya kuwa simu yenye kamera kubwa zaidi kuliko simu zote hadi sasa. Kwa mujibu wa tovuti ya Xiaomi, Note 8 inakuja kwa matoleo mawili tofauti ya Redmi Note 8 pamoja na Redmi Note 8 Pro

Xiaomi Redmi Note 8

Tukianza na Redmi Note 8, simu hii inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 6.3 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya LCD huku ikiwa na uwezo wa resolution ya Full HD+. Simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 13 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30fps.

Kwa nyuma Redmi Note 8 inakuja na kamera nne kamera kuu ikiwa na Megapixel 48, kamera nyingine zikiwa ni Megapixel 8 na kamera zilizobakia zote zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Kamera hizo zina uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 2160p@30fps sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za 4K. Mbali ya hayo simu hii inakuja na teknolojia za kamera za HDR pamoja na panorama.

Advertisement

Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Kwa upande wa sifa Redmi Note 8 ina endeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 665, processor inayo saidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 64, ukubwa huu unaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Xiaomi Redmi Note 8 ni kama zifuatazo.

Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Sifa za Xiaomi Redmi Note 8

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2 GHz, Quad-core, Kryo 260 + 1.8 GHz, Quad-core, Kryo 260).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 665.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 610.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili simu moja inakuja na RAM ya GB 4 na nyingine inakuja na RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/2.2, 1.25µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni ultrawide, pamoja na kamera mbili za Megapixel 2 ambazo ni dedicated macro camera na depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Blue, Black na Red.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Xiaomi Redmi Note 8 Pro

Kwa upande wa Redmi Note 8 Pro hapa ndipo mambo yanapokuwa mzuri zaidi, Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.53 kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku kikiwa na resolution ya 1080 x 2340 pixels. Kioo hichi kinakuja na ulinzi wa Gorilla Glass 5, ulinzi unaofanya kioo cha simu hii kuwa kigumu hasa pale kinapokutana na vitu vyenye uwezo wa kukwaruza au kupasua simu hiyo.

Simu hii inakuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 20 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps kwa kusaidiwa na teknolojia ya HDR.

Kwa nyuma Redmi Note 8 Pro inakuja na kamera nne ambapo kamera kuu inakuja na uwezo wa Megapixel 64, huku kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8 na mbili za mwisho zikiwa na uwezo wa Megapixel 2 kila moja. Simu hii kama ilivyo Note 8 nayo pia inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 2160p@30fps sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za hadi 4K.

Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Kwa upande wa sifa Redmi Note 8 Pro inakuja na processor mpya ya Mediatek Helio G90T (12nm) processor inayosaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128. Unaweza kuongeza ukubwa huo kwa kutumia Memory Card hadi ya GB 256. Sifa nyingine za Redmi Note 8 Pro ni kama zifuatazo.

Xiaomi Redmi Note 8 Pro Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 64

Sifa za Redmi Note 8 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2.05 GHz, Dual-core, Cortex A76 + 2 GHz, Hexa Core, Cortex A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek Helio G90T (12nm)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP4.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili Moja inakuja na ROM GB 64 na nyingine inakuja na ROM GB 128
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na RAM ya GB 4 na nyingine inakuja na RAM ya GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 68 yenye f/2.2, 1.25µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni ultrawide, pamoja na kamera mbili za Megapixel 2 ambazo ni dedicated macro camera na depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Red, Blue na White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Xiaomi Redmi Note 8 na Note 8 Pro

Kwa upande wa bei Redmi Note 8 inategemewa kuuzwa kwa nchini china kwa Yuan CNY999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 322,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa ROM GB 64. Toleo lenye GB 64 na RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan CNY 1199 sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 386,000 bila kodi

Kwa upande wa Redmi Note 8 Pro, simu hii inatarajiwa kupatikana kwa Yuan CNY1,399 ambayo ni sawa na shilingi 450,000 bila kodi kwa toleo lenye GB 6 na ROM GB 64. Kwa toleo lenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa GB 128 inategemewa kuuzwa kwa Yuan CNY 1799 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 580,000 bila kodi. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use