Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Simu hizi zimeongezewa Kamera pamoja na rangi zaidi
Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Kampuni ya Samsung siku ya leo imetangaza ujio wa simu mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s, simu ambazo ni matoleo ya maboresho ya simu za Galaxy A50 na Galaxy A30 zilizotoka mwaka huu 2019 takribani miezi sita iliyopita.

Kwa mujibu wa Samsung, simu hizo mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s zimefanyiwa maboresho mbalimbali ikiwa pamoja na maboresho ya kamera kwa simu zote mbili, pamoja na kuongezewa rangi zaidi ambapo simu hizi sasa zitakuwa zinapatikana kwa rangi nne mpya.

Advertisement

Samsung Galaxy A30s

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Tukianza na upande wa Galaxy A30s, simu hii haijafanyiwa maboresho makubwa zaidi ya kuongezewa kamera moja ya nyuma ambapo sasa inakuwa na kamera tatu ambazo ni Megapixel 25, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 5.

Mabadiliko mengine yaliyopo kwenye simu hii ni pamoja na resolution ya kioo cha Galaxy A30s imepunguzwa na sasa inakuja na resolution ya hadi pixel 720 x 1560 huku ikiwa na uwiano wa 19.5:9 ratio. Mbali na hayo sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo ilikuwa kwa nyuma sasa itakuwa inapatikana kwa mbele chini ya kioo. Sifa nyingine za simu hii ni kama ilivyo Galaxy A30.

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Sifa za Samsung Galaxy A30s

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~268 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7885 Octa (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G71.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 25 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2 huku kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya MicroUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Prism Crush Black, Prism Crush White, Prism Crush Green, na Prism Crush Violet 2.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Samsung Galaxy A50s

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Kwa upande wa Galaxy A50s nayo pia haina maboresho makubwa sana zaidi ya kamera za nyuma ambapo sasa zinakuja na uwezo mkubwa wa Megapixel 48, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 5. Kamera ya mbele nayo pia imeongezewa uwezo kutoka Megapixel 25 na sasa inakuja na Megapixel 32. Simu hii sasa inaweza kuchukua video za hadi 2160p@30fps au kwa lugha rahisi 4K kwa kutumia kamera zake za nyuma. Mbali na hayo Galaxy A50s haina tofauti zaidi na Galaxy A50.

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A30s na Galaxy A50s

Sifa za Samsung Galaxy A50s

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9610 Octa.
  • Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 128 na nyingine inayo GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/2.0, (wide), 1/2″, 0.8µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Prism Crush Black, Prism Crush White, Prism Crush Green na Prism Crush Violet2.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Galaxy A30s na Galaxy A50s

Kwa sasa bado Samsung haijatangaza bei za simu hizi, lakini tegemea kupata simu hizi kwa bei ghali zaidi kuanzia 750,000 kwa Galaxy A30s na Galaxy A50s tegemea kuipata kwa bei ya makadirio kuanzia Tsh 1,000,000. Kumbuka bei hizi ni makadirio hivyo bei hizi zinaweza kubadilika baada ya simu hizi kuzinduliwa hapa Tanzania.

Kupata habari zaidi kuhusu simu hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza pindi tu zinapo fika hapa Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use