Jinsi ya Kushare Picha Halisi Kutoka Instagram Kwenda Twitter

Njia hii itakusaidia kushare picha halisi na sio maandishi kama ilivyo sasa
Jinsi ya Kushare Picha Halisi Kutoka Instagram Kwenda Twitter Jinsi ya Kushare Picha Halisi Kutoka Instagram Kwenda Twitter

Wote tunajua kuwa instagram inakuja na sehemu ya kushare picha kwenda kwenye mitandao mingine ya kijamii, lakini mara nyingi kwa upande wa Twitter sehemu hii imekua ikifanya kazi kwenye maandishi pekee na sio picha au video unayo share kupitia Instagram.

Kupitia maujanja siku ya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ya kuweza kushare picha zako halisi na sio maandishi kutoka mtandao wa Instagram kwenda Twitter. Njia hii ni bora kwa sababu ukishafanya hatua hizi mara moja basi huto angaika tena bali utakuwa kila unachoweka kwenye akaunti yako ya mtandao wa Instagram, kinaenda moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Twitter bila wewe kufanya hatua nyingine za ziada. Bila kupoteza muda twende tukangalie njia hii.

Advertisement

Kwa kuanza pakua app inaitwa IFTTT, app hii inapatikana kwenye soko la Play Store na App Store na unaweza kupakua kupitia link hapo chini.

iOS Download Hapa

Baada ya kupakua na kuinstall app hii kwenye simu yako sasa endelea kwenye hatua hizi, fungua app hii kisha tengeneza akaunti kwa kutumia Google au Facebook. Baada ya hapo utaletwa kwenye uwanja wa App hiyo bofya sehemu ya kutafuta kisha andika Tweet your Instagrams utaona imetokea kadi yenye maneno Tweet your Instagrams as Native photos on Twitter.

Jinsi ya Kushare Picha Halisi Kutoka Instagram Kwenda Twitter

Chagua hiyo kisha bofya kitufe cha Connect kilichoko katikati ya ukurasa huo. Baada ya hapo utatakiwa kuunganisha akaunti yako ya Instagram, ukimaliza utatakiwa kuunganisha akaunti yako ya Twitter kisha moja kwa moja bofya kitufe cha Connect na utakuwa umemaliza.

Sasa kuanzia sasa kila picha utakayokuwa unapost kupitia mtandao wa Instagram itapostiwa pia kwenye mtandao wa Twitter ikiwa pamoja na maelezo pamoja na picha kamili. Huna haja ya kufanya kitu kingine kuanzia sasa kwani App hii itaendelea kupost kwenye akaunti yako ya Twitter kila siku utakapo kuwa unapost. Unaweza hata kuondoa App hiyo kwenye simu yako na huduma hii itaendelea kama kawaida.

Natumaini umeweza kushare picha zako kwenye akaunti yako ya Twitter, kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube ili ujifunze kwa vitendo, pia unaweza kusoma hapa kujifunza jinsi ya kuzuia meseji za promosheni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use