Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Galaxy Note 10 Kuachana na Tundu la Kuchomeka Headphone

Baada ya kampuni ya Apple sasa ni zamu ya kampuni ya Samsung
Samsung Galaxy Note 10 Kuachana na Tundu la Kuchomeka Headphone Samsung Galaxy Note 10 Kuachana na Tundu la Kuchomeka Headphone

Kwa muda sasa kampuni nyingi za kutengeneza simu au smartphone zimekuwa zikitoa simu mbalimbali bila sehemu ya kuchomeka headphone au headphone jack, lakini kwa muda wote huo kampuni ya Samsung imekuwa ikiendeleza utamaduni wa kutoa simu zenye sehemu ya kuchomeka headphone kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakipendelea.

Lakini siku za karibuni tegemea mabadiliko kutoka kampuni ya Samsung kwani kampuni hiyo imeanza kukubaliana na mabadiliko ya simu zisizo na tundu la kuchomeka headphone. Kwa mujibu wa tovuti ya TechCrunch, kampuni ya Samsung inatarajia kuzindua simu mpya ya Galaxy Note 10 bila sehemu ya tundu la kuchomeka headphone au headphone jack.

Advertisement

Taarifa hizi zinakuja baada ya kuvuja kwa picha ya kiunganishi cha waya ambacho kinasemekana ndio kitakuwa kinatumika kuunganisha headphone za zamani za kutumia pini na simu hiyo ya Galaxy Note 10.

Samsung Galaxy Note 10 Kuachana na Tundu la Kuchomeka Headphone

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Samsung kuja na simu yenye kutumia dongle au waya maalum kuunganisha headphone, kitu ambacho ni wazi kinachukiwa na watu wengi hasa kwenye nchi za Afrika kutokana na upatikianaji mgumu wa headphone ambazo hazitumii pini ya 3.5mm jack.

Kama kweli kampuni ya Samsung itakuwa imekubaliana na matokeo ya kuondoa simu zenye kutumia headphone jack, basi ni wazi kuwa siku za karibuni kampuni nyingine nazo zitaanza kubadilika na pengine hadi mwaka 2022 simu nyingi zitakuwa hazina sehemu hiyo maarufu.

Kwa sasa zimebaki siki sita tu hadi kuzinduliwa kwa simu mpya za Samsung Galaxy Note 10, hivyo ni wazi tutapata majibu ya taarifa hizi ndani ya siku chache zijazo. Kama bado hujafanikiwa kuona picha za muonekano wa Galaxy Note 10 unaweza kuziangalia kwa kusoma hapa. Pia kama unataka kujua sifa za awali za Galaxy Note 10 Plus unaweza kusoma hapa. Kwa habari zaidi kuhusu Galaxy Note 10 hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani tutakujuza yote ya muhimu kuhusu simu hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use