in

Ukweli Kuhusu App ya DENT, Je Inatoa Vocha za Bure au Utapeli.?

Je ni kweli kama app hii inauwezo wa kuchua salio lako kwenye simu..?

Ukweli Kuhusu App ya DENT, Je Inatoa Vocha za Bure au Utapeli.?

Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi na uhakika hadi sasa utakuwa unajua kuhusu App ya DENT, kama kwa namna yoyote wewe ni mgeni hapa basi unaweza kuendelea kusoma makala hii au unaweza kusoma makala yetu iliyopita ya jinsi ya kupata vocha za bure kwa kutumia App ya DENT.

Sasa kwa wale wenyeji hebu twende moja kwa moja kwenye mada husika kwani najua hilo ndio jambo lilio waleta wengi wenu. Kupitia makala hii utaenda kufahamu DENT ni nini na pia inakuaje app hii inatoa vocha za bure kwa watumiaji wa mitandao mbalimbali, vilevile kama hautochoka kusoma basi utaenda kujua jinsi ya kutumia app hiyo kikamilifu. Basi bila kupoteza let’s get to it.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

DENT ni nini

Kwa kuanza labda nikwambie DENT nini, Kwa mujibu wa tovuti ya bitcoin wiki DENT kwa jina kamili inaitwa DENT Coin, DENT Coin ni aina mpya ya pesa ya kidigital au cryptocurrency ambayo imejikita zaidi kwenye sekta ya data ya simu, lengo kubwa la pesa hii ya kidigital ni kuruhusu watumiaji kuweza kununua na kuuza data kwa kutumia mfumo wa kidigital unao julikana kama blockchain.

Kifupi ni kwamba DENT Coin ni kama Bitcoin, lakini zimetofautina kwani Bitcoin inaweza kubadilishwa kuwa fedha wakati DENT Coin haiwezi kubadilishwa kuwa fedha taslim bali unaweza kubadilisha na kuwa kiasi fulani cha data au salio la muda wa maongezi.

DENT Inamilikiwa na nani

Kwa mujibu wa tovuti ya coinswitch, DENT Coin pamoja na DENT App zote zimetengenezwa na kampuni inayoitwa DENT Wireless Limited ambayo iligunduliwa na Tero Katajainen, mwaka 2014 huko Hong Kong.

DENT Inafanyaje kazi

DENT inakuja na wazo zuri sana ambalo pengine linaweza kusaidia sana watu hasa nchi za Afrika ambapo watu wengi hutumia huduma za simu za Prepaid au malipo kabla ya matumizi. Sasa ili kuelewa kuhusu DENT labda nikueleze kwa kutumia mfano.

Oky…, fikiria labda wewe umesafiri kutoka Tanzania na umeenda nchini Afrika ya Kusini ukiwa na laini yako ya Vodacom au Tigo, kufika huko ukakuta gharama za kununua vifurushi vya internet pamoja na muda wa maongezi ni bei ghali sana au ni ngumu kupatikana kwa mitandao yako ya Vodacom au Tigo.

App ya DENT inakupa uwezo wa kununua Data pamoja na muda wa maongezi kwenda mitandao yako ya simu ya Vodacom au Tigo hata kama mitandao hiyo haiuzi vocha nchini Afrika ya Kusini. Hivyo basi, kama upo Tanzania na unatumia laini ya Vodacom ukiwa na app ya DENT unaweza kusafiri na laini yako kwenda nchi yoyote bila wasiwasi kuwaza utapata wapi salio la muda wa maongezi au bando la internet kwenye lain yako pale unapokuwa kwenye nchi nyingine.

Mbali na hayo kwenye baadhi ya nchi DENT inaruhusu watumiaji kuweza kuuza au kununua data na salio baina ya watumiaji, mtumiaji ataweza kuuza data au salio kwa kiasi cha DENT Coin anazotaka ili kuweza kupata faida. Unaweza kununua DENT Coin kwa kutumia pesa lakini hutoweza kubadilisha DENT Coin kuwa pesa bali utaweza kubadlisha DENT Coin kuwa salio au kiasi fulani cha bando.

Je ni Kweli DENT inatoa vocha za bure

Kutokana na uzoefu wangu baada ya kutumia App hii ni kuwa, DENT inatoa DENT Coin ambazo hizi unaweza kubadilisha na kuwa bando au salio la muda wa maongezi. Ili kupokea bando au salio ni lazima uwe umeweka namba yako ya simu wakati wa kujisajili au ni lazima kujua namba ya mtu ambaye ndio unamtumia salio hilo. DENT haiweki salio hilo kwenye huduma za kifedha kama M-Pesa au Tigo Pesa bali unapokea salio kwenye namba yako ya simu kama mtu anapo kununulia salio kutoka benki.

Kwa nini DENT inatoa Vocha za Bure

DENT kama biashara nyingine mtandaoni inafanya promosheni ili kuvutia watumiaji wake, kupitia app ya DENT unaweza kushiriki link yako na ndugu na jamaa na pale watakapo pakua app ya DENT kwa kutumia link hiyo wote mtaweza kupokea kiasi fulani cha DENT Coin ambacho kinaweza kutumika kununua muda wa maongezi au bando kupitia app ya DENT.

Mfumo huu ni kama ule ambao mtumiaji anapewa promo code ambayo mtumiaji mpya anapo tumia promo code hiyo basi mwenye promo code anapokea kiasi fulani cha pesa na aliye alikwa au mtumiaji mpya anapewa punguzo kwenye huduma anayotumia.

Tofauti na promosheni nyingine mfumo wa kualika marafiki kwenye DENT unaenda ukibadilika na kwa mujibu wa tovuti ya DENT, promosheni ya kualika marafiki inaweza kuisha muda wowote au kusitishwa kwa mtumiaji kutokana na sababu mbalimbali, Vilevile kiasi cha DENT Coin unachopokea kwa kumualika mtu ni tofauti kulingana na muda.

Je DENT ni App ya kitapeli

Kwa mujibu wa nyaraka kutoka kampuni ya DENT Wireless LTD, DENT ni kampuni iliyo sajiliwa na inafanyakazi kialali kabisa. App hiyo pia imekwepo kwa muda kidogo kuanzia mwaka 2018 ambapo app za Android na iOS ndipo ziliwekwa kwenye masoko ya Play Store na App Store. Pia app ya DENT imekuwa ikishirikiana na kampuni kubwa za simu duniani kuhakikisha huduma zake zinawafikia watumiaji kote duniani.

Ukweli Kuhusu App ya DENT, Je Inatoa Vocha za Bure au Utapeli.?

Je App ya DENT ni salama

Hakuna mtu anayeweza kusema programu yoyote ni salama kwa asilimia 100, chochote kinaweza kutokea kutokana na kuwa wote sisi ni watumiaji wa kawaida na hakuna namna ambapo tunaweza kusema app yoyote ni salama ijapokuwa sisi yani mimi na wewe wote sio watengenezaji wa programu husika.

Hivyo basi sisi kama Tanzania Tech hatuna uhakika kama programu DENT ni salama kwa asilimia 100 hivyo ni vizuri kutadhimini mwenyewe na kutoa uamuzi wa kutumia au kuacha kutumia App hiyo. Lakini pia tumeandika barua pepe kwa kampuni husika tukitaka kujua usalama wa app hiyo hivyo pale tutakapo jibiwa tutarudisha majibu kwenu ili wote kwa pamoja tuweze kujua.

Kama umefanikiwa kusoma hadi hapa basi nakupa ongera na natumaini kwa sasa umeelewa kuhusu app ya DENT, Kwetu sisi ni muhimu sana kutoa ufafanuzi kama huu kwani pia tunapenda kuwa makini pale tunapokupa habari au maujanja yenye uhakika na ambayo yanaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine. Hivyo basi kama una mahali ambapo hujaelewa basi unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Ukweli Kuhusu App ya DENT, Je Inatoa Vocha za Bure au Utapeli.?
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.