Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

Zifahamu kwa undani hizi hapa sifa na bei ya Xiaomi Mi CC9 na CC9e
Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

Kampuni ya Xiaomi hivi karibuni imeongeza series mpya kwenye simu zake, Xiaomi CC ni toleo jipya kabisa la simu mpya za Xiaomi ambazo zitakuwa zinalenga watumiaji wa daraja la kati. Kupitia series hiyo mpya kampuni hiyo imekuja na simu mpya za Xiaomi CC9 na CC9e.

Tukianza na Xiaomi CC9, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.39 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED ambacho pia kinakuja na resolution ya hadi pixel 1080 x 2340. Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama water drop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya Selfie ya Megapixel 32.

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

Advertisement

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu ambapo kamera kubwa inakuja na Megapixel 48, huku nyingine zikiwa na Megapixel 8 na nyingine ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote zinakuja na uwezo wa kurekodi video za hadi 4k pamoja na 1080p.

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

Mbali na kamera, simu hii inaendeshwa na processor ya Snapdragon 710 chipset processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa hadi GB 64 au GB 128, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa memory card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Xiaomi CC9 ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi CC9

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (10 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na ROM ya GB 64 na nyingine ikiwa na ROM ya GB 128, Simu zote mbili zina uwezo wa kuongezwa na memory card ya hadi microSD ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye uwezo wa HDR
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8, ultra wide na nyingine ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4030 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth ya 5.0, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue, White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Xiaomi CC9

Kwa upande wa bei Xiaomi CC9 inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia tarehe 5 huko nchini china na inategemewa kuuzwa kwanza kwa nchini china kwa Yuan CNY 1,799 ambayo ni sawa na Tsh 602,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ROM ya GB 64. Toleo lenye RAM ya GB 8 na ROM ya GB 128 itauzwa kwa Yuan CNY 1,999 ambayo ni sawa na Tsh 669,000 bila kodi.

Simu nyingine kwenye Series ya simu za Xiaomi CC ni CC9e, Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.01 kioo ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED ambacho pia kinakuja na resolution ya hadi pixel 720 x 1560. Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa water drop notch ambao unahifadhi kamera ya selfie ya Megapixel 32.

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

Mbali na hayo Xiaomi CC9e haina tofauti kabisa na Xiaomi CC9 zaidi ya kuwa na processor ya Qualcomm SDM665 Snapdragon 665 yenye speed ya Octa-core 2.0 GHz Kryo 260 pamoja na GPU ya Adreno 610. Sifa kamili za Xiaomi CC9e ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi CC9e

Xiaomi Yazindua Simu Mpya za Mi CC9 pamoja na Mi CC9e

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.01 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Kryo 260
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM665 Snapdragon 665 (11 nm)
  • Uwezo wa GPU – Adreno 610.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na ROM ya GB 64 na nyingine ikiwa na ROM ya GB 128, Simu zote mbili zina uwezo wa kuongezwa na memory card ya hadi microSD ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye uwezo wa HDR
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8, ultra wide na nyingine ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4030 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth ya 5.0, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue, White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Xiaomi CC9e

Kwa upande wa bei Xiaomi CC9e inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia tarehe 5 huko nchini china na inategemewa kuuzwa kwanza kwa nchini china kwa Yuan CNY 1,299 ambayo ni sawa na Tsh 435,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ROM ya GB 64. Toleo lenye RAM ya GB 8 na ROM ya GB 64 itauzwa kwa Yuan CNY 1,599 ambayo ni sawa na Tsh 535,000 bila kodi. Toleo la RAM ya GB 8 na ROM ya GB 128 bado haijajulikana itauzwa kwa bei gani.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use