Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya simu mpya ya TECNO phantom 9

Kama wewe ni mpenzi wa simu za TECNO basi habari njema kwako kwani kampuni ya TECNO hivi karibuni imezindua rasmi simu mpya ya TECNO Phantom 9 huko nchini Nigeria. Simu hii ni toleo jipya la simu za Phantom, Simu ambazo ndio simu zenye sifa bora zaidi kwenye matoleo yote ya simu za TECNO.

Kama ilivyokuwa kwenye tetesi, simu hii inakuja na sifa sawa kabisa na zile zilizotangazwa kwenye makala iliyopita. Kwa ufupi, TECNO Phantom 9 inakuja na kioo kikubwa cha Inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED kioo ambacho pia kina resolution ya hadi pixel 1080 x 2340.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa juu ambao una julikana kama water drop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele ya Selfie ya Megapixel 32, kamera hiyo inasaidiwa na Flash mbili zilizopo kwa mbele karibia na kona za simu hiyo. Vilevile kwenye kioo hicho kunakuja teknolojia mpya ya Fingerprint ambayo inaruhusu mtumiaji kufunga simu yake kwa kutumia alama za vidole.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Kwa nyuma, TECNO Phantom 9 inakuja na kamera tatu ambazo zina Megapixel 16, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 2, kamera zote zinasaidiwa na teknolojia ya AI pamoja na HDR pamoja na teknolojia nyingi ambazo zitafanya picha zako kuonekana vizuri sana.

Jiandae na Simu Zenye Kamera ya Mbele Inayojificha Chini ya Kioo

Kwa upande wa sifa za ndani Phantom 9 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm), yenye CPU ya Octa-core 4×2.35 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53). Procesor hii inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huu unaweza kuongezwa na memory card ya MicroSD Card ya hadi ya GB 500.

Pia TECNO Phantom 9 itakuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie), mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa Tecno HiOS v5.0, Sifa nyingine za TECNO Phantom 9 ni kama zifuatazo.

Sifa za TECNO Phantom 9

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.35 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53)
 • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm).
 • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 500.
 • Ukubwa wa RAM – GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
  na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Aurora Blue.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G

Bei ya TECNO Phantom 9

Kwa mujibu wa TECNO, Kwa upande wa bei simu hii mpya inatarajiwa kuingia sokoni hapa Tanzania siku za karibuni, Na inategemewa kupatikana kwa bei ya makadirio kuanzia shilingi za kitanzania Tsh 750,000 hadi Tsh 720,000 Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na mahali unapo nunua simu hii.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.