Zimebaki wiki chache hadi kuzinduliwa kwa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 10, simu ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 7 ya mwezi wa nane siku ya jumatano huko nchini marekani. Lakini kabla ya simu hiyo kutoka rasmi hivi leo kumevuja picha ambazo inasemekana kuwa ndio muonekano halisi wa Samsung Galaxy Note 10.
Kwa mujibu wa tweet kutoka kwa mvujisha maarufu Ishan Agarwal, Galaxy Note 10 itakuja ikiwa na rangi tofauti ikiwemo nyeusi (black) na silver yenye mchanganyiko wa rangi ya blue (gradient color).
Kwa upande wa muonekano kama unavyoweza kuona Galaxy Note 10 inakuja na kioo kikubwa huku kikiwa na kamera ya mbele moja ambayo ipo juu ya kioo, kwa nyuma Galaxy Note 10 inakuja na kamera tatu huku Galaxy Note 10 Plus ikija na kamera nne kwa nyuma.
Kwa mujibu wa tetesi hizo Galaxy Note 10 na Note 10 Plus zote zinasemekana kuja na sehemu ya Fingerprint chini ya kioo kama zilivyo simu mpya za Galaxy S10 na S10 Plus. Kwa sasa hayo ndio machache unaypo julikana kuhusu simu hizi mpya za Galaxy Note 10 na Note 10 Plus.
Kujua zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembela tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu YouTube ili kupata kujua yaliyomo kwenye simu hiyo mpya.
Safi sana lakini muwe mnaweka bei za simu zote ili kuwapa watu fahamu na tamaa ya kununua