Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Njia 5 zinazoweza kukusaidia kutumia app ya telegram kwa urahisi
Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Telegram ni moja kati ya App bora sana ya kuchat hivi sasa, app hii imekuwa bora kutokana na usalama wake pamoja na kuwa na sehemu nyingi nzuri ukitofautisha na app ya WhatsApp ambayo kwa sasa inatumiwa na watu wengi zaidi.

Najua kuna baadhi ya watu watakuwa wanapingana na mimi lakini kwa leo hebu tufanye topic ya ubora kati ya Telegram na WhatsApp iwe ya siku nyingine, Kwa leo hebu twende tukaangalie njia 5 ambazo huenda ulikuwa uzijui ambazo zinaweza kusaidia kurahisishia matumizi ya app yako ya Telegram.

Jinsi ya Kuzima Kuonekana kwa Meseji Unapochati

Mara nyingi unapo pokea meseji wakati unachati kwa kutumia app ya Telegram utaweza kuona meseji yenyewe ikionekana kwa juu kwenye simu yako hata kabla ujafungua meseji yenyewe, sehemu hii huwa inaitwa (Message Preview). Sehemu hii ipo kwa ajili ya kurahisha kuangalia kama meseji ni muhimu kusoma kwa muda huo au lah.., hata hivyo kuna wakati sehemu hii inakuwa kama chanzo cha mtu kusoma meseji zako kutokana na kuweza kuonyesha wazi sehemu ya meseji yako.

Advertisement

Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Sasa ili kuweza kuzima sehemu hii unaweza kufuata hatua hizi fupi, bofya sehemu ya Settings kisha utafunguka ukurasa wenye profile yako kama unavyonekana hapo juu bofya sehemu ya Notification and Sounds kisha chagua Private Chat alafu zima sehemu ya Message Preview.

Jinsi ya Badilisha Rangi ya Mwanga wa Notification

Kama simu yako inayo sehemu ile yenye taa ambapo meseji ikingia inawaka basi njia hii inaweza kuwa nzuri sana kwako, kupitia app ya Telegram unaweza kubadilisha rangi ya mwanga unaowaka pale meseji ya telegram inapoingia.

Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Ili kuweza kubadilisha rangi ya taa hiyo unachotakiwa kufanya bofya sehemu ya Settings kisha utafunguka ukurasa wenye profile yako kisha bofya sehemu ya Notification and Sounds kisha chagua Private Chat au Group au Channel inategemeana na sehemu unayotaka kuweka rangi hiyo kisha bofya sehemu ya LED Color, baada ya hapo chagua jina la rangi kama unavyotaka.

Jinsi ya Kuzuia Picha na Video Kudownload Zenyewe

Ni wazi kuwa bando imekua ni tatizo kwa watu wengi sana, japokuwa zipo njia za kipata vocha za bure lakini sio kila mtu anayeweza kufanya njia hizo. Sasa ili kuzuia bando lako kuisha kwa haraka tena hasa pale unapokuwa na group lenye kutuma picha na video mara kwa mara ni vyema kuzuia picha na video kujidownload zenyewe kupitia app ya Telegram.

Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Ukiwa kwenye ukurasa wa Settings, bofya sehemu ya Data and Storage kisha utaona sehemu iliyo andikwa Automatic media download, chini yake zima sehemu zote mbili za Mobile data na Wi-Fi.

Jinsi ya Kuzima Sehemu ya Last Seen

Kama ilivyo app ya WhatsApp telegram nayo inakuja na mfumo ambao unaweza kuonyesha kama unapatikana hewani kwa sasa yaani Online, au kama ulingia kwenye app hiyo muda mfupi uliopita au Last Seen. Kwa watu wengine sehemu hii huwa haitajiki ndio maana unaweza kuzima sehemu hii kwa kufuata njia hizi rahisi.

Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Ukiwa bado uko kwenye ukurasa wa Settings, bofya sehemu ya Privacy and Security, kisha chini ya Privacy utaona sehemu ya Last Seen & Online bofya hapo alafu chagua Nobody alafu bofya tiki iliyopo juu upande wa kulia.

Jinsi ya Kuweka Password kwenye Chat Zako Zote

Kupitia app ya Telegramu utaweza kuweka password kwenye kila chat ambayo unachat na hii inaweza kukusaidia sana kuzuia watu kusoma meseji zako hasa pale ambapo hujui. Sasa ili kuweza kuweka password kwenye chat zako fuata hatua hizi.

Maujanja ya Kuwezesha Kutumia App ya Telegram Kikamilifu

Ukiwa bado kwenye ukurasa wa Privacy and Security, bofya sehemu ya Passcode Lock ambayo ipo chini ya sehemu ya Security, baada ya hapo washa sehemu hiyo kwa kubofya switch kwenye sehemu iliyopo kulia juu baada ya hapo weka password unayotaka kutumia kisha bofya sehemu ya tiki iliyopo kwa juu kulia.

Na hayo hizo ndio njia ambazo unaweza kutumia na kuongeza ufanisi wa app ya telegram. Kumbuka njia hizi zinaweza kutofautina kwenye app ya Telegram X hivyo kama unataka maujanja kupitia app ya telegram x unaweza kuandika kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use