Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai

Zifahamu sifa na bei ya awali ya simu hii kabla haijazinduliwa rasmi
TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai

Mwaka jana 2018 kampuni ya TECNO haikuzindua toleo jipya la simu za Phantom, lakini mwaka huu mambo ni tofauti kwani kampuni hiyo inatarajia kuzindua simu mpya ya TECNO Phantom 9 mwanzoni mwa mwezi julai.

Kwa mujibu wa ripoti za uhakika, simu hiyo mpya ya Phantom 9 inatarajiwa kuja na muundo wa kisasa pamoja na sifa bora kuliko matoleo yote ya simu za Tecno Phantom. Simu hiyo mpya ya Phantom 9 inatarajiwa kuja na kioo kikubwa chenye kutumia teknolojia ya AMOLED tofauti na simu nyingi za tecno ambazo hutumia vioo vyenye teknolojia ya IPS LCD.

Advertisement

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai

Mbali na teknolojia mpya ya kioo, Phantom 9 pia ndio itakuwa simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya tecno kuwa na sehemu ya ulinzi ya Fingerprint chini ya kioo. Kwa kuchanganya teknolojia hiyo ya kioo pamoja na sehemu hiyo ya Fingerprint ni wazi kuwa TECNO Phantom 9 itakuwa ni simu bora kuliko simu zote za tecno hadi sasa.

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai

Mbali na hayo yote, simu hii mpya ya Phantom 9 pia inakuja na kamera nzuri sana zenye teknolojia ya AI, huku kwa mbele simu hii ikuwa inakuja na kamera ya selfie ya Megapixel 32, kamera ambayo inasaidiwa na teknolojia ya AI pamoja na Flash mbili ambazo zitasaidia kufanya picha zionekane zikiwa na mwanga bora hata kama ni wakati wa usiku. Hata hivyo kamera hiyo imewekwa kwenye ukingo wa juu maarufu kama water drop notch huku flash hizo mbili za mbele zikiwa zimefichwa kwa mbele juu karibia na pembe za simu hiyo.

Kwa nyuma TECNO Phantom 9 inakuja na kamera tatu za Megapixel 16, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 2 huku kamera zote hizo zikiwa na teknolojia ya AI pamoja na flash nne za LED au Quad-LED. Kamera ya simu hii inakuja na teknolojia nyingi za kufanya picha ziwe bora, kama vile teknolojia za HDR pamoja na Panorama.
TECNO Kuzindua Simu Mpya ya TECNO Phantom 9 Mwezi Julai

Kwa upande wa sifa za ndani Phantom 9 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm), yenye CPU ya Octa-core 4×2.35 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53). Procesor hii inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huu ukiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya MicroSD Card ya hadi ya GB 500.

Vilevil TECNO Phantom 9 itakuja na mfumo wa Android 9.0 (Pie), mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa Tecno HiOS v5.0. Hata hivyo vitu vyote vilivyopo ndani ya siku hiyo vitakuwa vinaendeshwa na battery ya Li-ion yenye uwezo wa 3500 mAh, batter ambayo itafanya simu hiyo kudumu na chaji kwa angalau siku moja nzima kulingana na matumizi yako.

Inasemekana kuwa simu hii pia itakuja na teknojia ya Fast Charge lakini pengine tusubiri mpaka simu hii itakapo zinduliwa rasmi hapa Tanzania ili kusudi tuweze kujaribu na kujua zaidi kuhusu hilo.

Kuhusu bei inasemekana TECNO Phantom 9 itakuja ikiwa inauzwa kwa hadi Shilingi Tsh 850,000 au zaidi hapa Tanzania, huku bei hiyo ikiwa imejumuisha na kodi. Ni wazi kuwa simu hii itazinduliwa kwa ushirikiano na Tigo kwa hapa Tanzania hivyo tegemea kupata ofa za bando pale simu hii itakapo zinduliwa. Kumbuka bei iliyotajwa hapo juu inaweza kubadilika baada ya simu hii kuzinduliwa rasmi hapa Tanzania.

Kwa sasa hayo ndio machache kuhusu simu hiyo mpya ya Phantom 9, ili kujua zaidi kuhusu yaliyomo ndani ya simu hiyo hakikisha una tembelea channel yetu ya YouTube ya Tanzania Tech hapa tutakujuza zaidi ikiwa pamoja na mahali unapo weza kununua simu hii kwa punguzo pale itakapo zinduliwa rasmi hapa Tanzania.

2 comments
  1. Ni bonge la simu. Tecno wanakimbiza mwizi kimya kimya.Makampuni mengine ya kutengeneza simu yatakoma. Mchina hana mzaha apo mbele kamtanguliza Huawei.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use