Kampuni ya Nokia hivi leo imerudi sokoni na simu mpya ya Nokia 2.2 ambayo inakuja ikiwa inauzwa kwa bei nafuu sana. Mbali ya kuwa bei nafuu, Nokia 2.2 inakuja na sifa nzuri ambazo ni bora kwa watumiaji wengi wa simu za Android.
Tukianza na kioo, Nokia 2.2 inakuja na kioo cha inch 5.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD kioo ambacho kina resolution ya hadi pixel 720 x 1520. Kwa juu kioo hicho kina kuja na ukingo wa juu ambao unahifadhi kamera ya mbele ya Megapixel 5.
Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 13 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080, kamera hiyo ya nyuma inasaidiwa na flash ya LED ambayo inasaidia kufanya picha ziwe na mwanga bora hasa wakati wa usiku. Mbali na hayo simu hii haina sehemu ya fingerprint hivyo inakuja na ulinzi wa kutambua uso au Face Unlock.
Nokia 2.2 ina endeshwa na processor ya Mediatek MT6761 Helio A22, huku ikisaidiwa na RAM ya GB 2 au GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 16 na GB 32. Hata hivyo ukubwa huu unaweza kuongezwa kwa memory card ya Micro SD yenye uwezo wa hadi GB 400.
Simu hii inaendeshwa na mfumo wa Android 9.0 Pie, mfumo ambao juu unakuja na mfumo wa Google wa Android One. Sifa nyingine za Nokia 2.2 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Nokia 2.2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~295 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm) Chipset.
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 16 na nyingine inakuja na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 2 na nyingine ikiwa na GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/2.2, 1/3″, 1.12µm, AF huku ikiwa inasadiwa na Flash ya LED flash, panorama, na HDR.
- Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, Hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa mbili za Steel na Tungsten Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za accelerometer na proximity
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Ulinzi wa Kutambua Uso (Face ID). Haina Fingerprint
Bei ya Nokia 2.2
Kwa mujibu wa Nokia, Simu hii inasemekana kuanza kupatikana hivi karibuni kuanzia dollar za marekani $100 sawa na takribani Tsh 230,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 2 na ukubwa wa ndani wa GB 16. Toleo lenye GB 32 na RAM ya GB 3 litauzwa kwa dollar za marekani $115 sawa na takribani Tsh 265,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.
tupe taarifa ikifika nchini
Naombeni detail za Nokia 3.2