in

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Milioni 13 ni kompyuta yenyewe na Milioni 11 ni kioo cha kompyuta hiyo

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Kupitia mkutano wa WWDC 2019, kampuni ya Apple imetangaza ujio wa kompyuta mpya ya Mac Pro ambayo inasemekana kuwa na nguvu kuliko kompyuta zote za Mac na Macbook Pro. Mbali ya kuwa kompyuta yenye nguvu kuliko zote pia Mac Pro inasemekana kuwa ndio kompyuta ya bei ghali kuliko kompyuta zote za Apple zilizotoka hadi sasa.

Muundo wa Mac Pro

Tukianza na kompyuta yenyewe, Mac Pro imetengenezwa kwa mtindo mpya na wakisasa ambao unafanya kompyuta hiyo kuonekana vizuri, moenekano huo pia umezingatia sana upande wa kupooza kompyuta hiyo kwani Mac Pro imetengenezwa maalum kwa ajili ya kazi.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Kama unavyoona kwenye picha hapo juu, Mac Pro inakuja na matundu kwa nyuma na mbele matundu ambayo hutumika kupooza kompyuta hiyo pale inapokuwa inafanya kazi zaidi. Mbali na hayo kwa mbele ndani kwenye eneo hilo kompyuta hiyo inakuja na feni za kisasa ambazo Apple inadai kuwa hazitoi mlio kabisa hasa kompyuta hiyo ikiwekwa chini ya meza. Feni hizo zitasaidiana na upepo wa kawaida unaopitia kwenye matundu hayo kupooza kompyuta hiyo.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Sifa za Mac Pro

Kwa sababu kompyuta hii imetengenezwa na fikra za kuipooza zaidi ni wazi kuwa kompyuta hii inakuja na uwezo mkubwa. Kwa mujibu wa Apple Mac Pro inakuja na processor yenye uwezo wa mkubwa sana wa hadi 28-core, processor ambayo ni Intel Xeon W processor. Mac Pro pia inauwezo wa kuimili RAM hadi Terabyte TB 1.5, pamoja na SSD ya hadi Terabyte 4. Haija ishia hapo Mac Pro inakuja na uwezo mkubwa sana wa graphics ambapo inaweza kuimili graphics card nne za AMD Radeon Pro Vega II Duo GPU, hizi ni nzuri sana kwa wabunifu wa michoro pamoja na watengenezaji wa sinema za hadi 8k.

Mbali na hayo, Mac Pro imetengenezwa ikiwa na sehemu nyingi zaidi za kuchomeka vifaa vya kuongeza uwezo kompyuta hiyo, huku ikiwa na sehemu nane za kuchomeka PCI Express card, sehemu mbili za kuchomeka USB-C / Thunderbolt 3, sehemu mbili za kuchomeka USB-A huku sehemu nyingine mbili za USB-C zikiwa kwa juu ya kompyuta hiyo.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Mbali na hapo Apple imekuja na aina mpya ya kifaa ambacho kinatumika kuongeza uwezo zaidi wa kompyuta hii, kifaa hicho ambacho kinaitwa MPX Module, kina chomekwa kwenye sehemu tatu za Thunderbolt ambazo zipo ndani ya motherboard ya kompyuta hiyo. Kifaa hicho kinatumika kuchomeka graphics card mbili kubwa ambazo zinaweza kuongeza uwezo zaidi wa kompyuta hiyo, kuthirisha uwezo wa kifaa hicho, kifaa hicho kina kuja na feni yake yenyewe ambayo hupooza card hizo zinapo fanya kazi zaidi.

Vilevile pia Apple inakuja na kadi nyingine ya I/O module, ambayo hii inakuja na sehemu nyingine mbalimbali za kuchomeka Thunderbolt 3 ports, sehemu nyingine mbili za USB-A ports, sehemu ya kuchomeka headphone 3.5mm audio jack, pamoja na sehemu ya kuchomeka video card ambayo inatumia  FPGA kuprocess hadi pixel bilioni 6 kwa sekunde.

Bei ya Mac Pro

Kwa mujibu wa Apple Mac Pro inategemea kuingia sokoni kuanzia mwezi wa nane, huku bei yake ikianzia dollar za marekani $5,999 sawa na takribani Tsh milioni 13.7 bila kodi. Hata hivyo bei hiyo ni kwa kompyuta hiyo yenye uwezo wa RAM ya GB 32, processor ya octa-core Intel Xeon CPU, Graphics card ya Radeon Pro 580X, pamoja na SSD ya GB 256. Kama unataka uwezo zaidi unaweza kununua vitu vingine pembeni kutoka Apple.

Kioo cha Pro Display XDR

Sambamba na kompyuta hiyo, Apple imezindua kioo ambacho kinaweza kutumika na kompyuta hiyo, kioo ambacho kinauzwa tofauti na kompyuta hiyo. Kioo hicho cha LCD kinakuja na ukubwa wa inch 32 huku kikiwa na uwezo wa resolution ya hadi 6K ambayo ni sawa na pixel 6016 x 3384.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Kioo hicho kilichopewa jina la Pro Display XDR, kinakuja na stendi maalum ambayo nayo inauzwa pekee ambayo inaweza kufanya kioo hicho kutumika kikiwa kime simamishwa wima.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13

Kioo hicho kinasemekana kuja na waya za Thunderbolt 3 cable, ambazo hizi zinaweza kutumika kuunganishwa kwenye kompyuta Mac Pro, ambapo inasemekana unaweza kuunganisha hadi vioo sita vya aina hiyo kwa kutumia kompyuta hiyo ya Mac Pro.

Bei ya Pro Display XDR

Kioo hicho kinategemewa kuingia sokoni miezi michache ijayo, huku bei yake ikisemekana kuanzia dollar za marekani $4,999 ambayo hii ni sawa na takribani Tsh Milioni 11.2 bila kodi. Kwa upande wa stendi ya kioo hicho inasemekana kupatikana kwa dollar za marekani $999 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,295,000 bila kodi.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, ukitaka kompyuta hii ikiwa kwenye ubora pamoja na kadi zake zote na RAM ya TB 1 na SSD ya TB 4 pamoja na kioo hichi na stendi yake, basi jiandae kulipa dollar za marekani $35,000 ambayo ni sawa na takribani zaidi ya Tsh Milioni 80 bila kodi.

Na hiyo ndio kompyuta mpya ya Mac Pro pamoja na kioo chake cha Pro Display XDR vilivyo zinduliwa hapo siku ya jana kwenye mkutano wa WWDC. Kama unataka kujua zaidi kuhusu mengine yaliyo tangazwa kwenye mkutano huo basi tembelea ukurasa wetu maalum wa WWDC 2019 Hapa.

Apple Yaja na Mac Pro Kompyuta ya Gharama ya Zaidi ya Tsh Milioni 13
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.