in

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M40

Zifahamu kwa undani hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya Galaxy M40

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M40

Kama ilivyo semekana awali, hatimaye Samsung leo imezindua toleo jipya la simu za Galaxy M. Galaxy M40 ni simu inayokuja ikiwa na mtindo wa kisasa wa tobo maalum la kamera iliyopo ndani ya kioo, pamoja na kamera tatu kwa nyuma.

Galaxy M40 inakuja na kioo cha inch 6.3, kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku kikiwa na uwezo wa kuhimili hadi resolution ya pixel 1080 x 2340. Kwa mbele Galaxy M40 inakuja na kamera ya Megapixel 16 ambayo inayo teknolojia ya HDR, pamoja na uwezo wa kurekodi video za hadi pixel 1080 kwa sekunde 30 kila fremu (1080p@30fps).

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M40

Kwa nyuma Galaxy M40 inakuja na kamera tatu, kamera moja inakuja ikiwa na uwezo wa Megapixel 32, nyingine inakuja na Megapixel 8 na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 8. Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za 4K pamoja na 1080p.Mbali na kamera simu hii kwa nyuma inakuja na sehemu ya kufungua simu kwa alama za vidole maarufu kama Fingerprint scanner.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M40

Tuki achana na muonekano wa nje, Kwa ndani Galaxy M40 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 675 ambayo inasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 6 na GB 4, pamoja na ukubwa wa ROM wa kuchagua kati ya GB 128 na GB 64. Ukubwa huu unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory card ya hadi Terabyte 1. Sifa nyingine za Galaxy M40 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy M40

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.3 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~409 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz Kryo 460 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 460 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM675 Snapdragon 675 (11 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 612.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na ukubwa wa 64 na nyingine inakuja na ukubwa wa GB 128, simu zote mbili zinakuja na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na RAM ya GB 4 na nyingine inakuja na RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 32 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 3500 mAh, pamoja na teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Sweater Blue na Midnight Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy M40

Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy M40 itaanza kupatikana kwa nchini India siku ya tarehe 18 mwezi huu, na itakuwa inapatikana kwa bei ya kuanzia ya dollar za marekani $288 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania Tsh 662,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Na hiyo ndio simu mpya ya Galaxy M40, Kama umegundua simu hii inafanana sana kwa sifa na simu mpya ya Samsung Galaxy A60, simu ambayo nayo haina muda mrefu toka kuingia sokoni. Kama unataka kuona tofauti ya simu hizi mbili yaani Galaxy M40 na Galaxy A60 bofya hapa.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M40
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.